Ads 468x60px

Pages

Monday, March 22, 2010

TANGAZO

Kuhusiana na matatizo yaliyotokea hivi karibuni maeneo ya Hennur uongozi wa TASABA chini ya Rais Fidelis Msomekela ulifikia makubaliano pamoja na jeshi la polisi la Bangalore pamoja na mwakilishi wa ubalozi wetu Mh.Amon Mwamunenge kuhusiana na kuongeza ulinzi kwa wanafunzi wakitanzania waishio Bangalore.
Kutokana na hilo uongozi wa TASABA unasisitiza wanafunzi ambao hawajajiandikisha majina yao na kuchukua kitambulisho cha uanachama cha TASABA, watakua kwenye wakati mgumu wakipatwa na matatizo kwa sababu uongozi wa TASABA hauna taarifa zao rasmi kuhusu maeneo wanayokaa na namna ya kuwafikia. Hivyo watanzania wote waishio Bangalore wameombwa kujiandikisha na kuchukua fomu haraka iwezekanavyo kwa viongozi wao wa maeneo.Hii ni kwa wote ambao hawana kitambulisho cha TASABA mpaka hivi sasa.
TASABA SPOKESMAN
JUMANNE MTAMBALIKE

UFUMBUZI WA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA MOTO KWA WANAFUNZI.

Wanafunzi wawili ambao ni Ndugu. Hamis Mbelwa Fintan na Ndugu.Olais Alexendra Siarra, waliokuwa wanakaa Hennur Cross ambao walikutwa na mkasa wa kuchomewa moto nyumba yao wakiwa ndani umepatikna ufumbuzi baada ya Ubalozi wa Tanzania nchini India kuingilia kati sula hilo. tarehe 18/03/2010 Mh. A.M.R Mwamanenge kutoka ofisi za ubalozi wa Tanzania New delhi- India aliwasili jijini Bangalore. Majira ya 1:00pm siku hiyo hiyo tulifika katika kituo cha polisi cha Hennur Cross tukiongozana na Mh. A.M.R Mwamanenge na kuonana na Inspekta wa kituo hicho ambaye alitupa maafisa wawili wa polisi ambao tulifika nao sehemu ya tukio ili kujionea wenyewe kilichokuwa kimetokea na hatimaye kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha kituo cha polisi cha Hennur Cross. Watuhumiwa walipohojiwa hawakuwa na sababu ya msingi ya kueleza kisa kilicho wapelekea kufanya kitendo walichokifanya zaidi ya kuomba msamaha na kudai kuwa walikuwa wamelewa siku hiyo. Walikili kosa mbele ya Inspekta wa kituo hicho kimaandishi kuwa hawatarudia tena kosa hilo na pia kama itatokea tukio lingine kwa kipindi hiki basi wao ndio watakuwa watuhumiwa wa kwanza.
Ili kuweka hali ya amani na utulivu nikiwa kama mwenyeketi wa jumuiya ya waTanzania waishio Bangalore pamoja na wahanga wa tukio hilo tulimwomba Mh. A.M.R Mwamanenge tulimalize tatizo lile kwa njia ya diplomasia kwa kuwa kuwafungulia kesi na kuwapandisha mahakamani ingeweza kuleta mgogoro zaidi na wenyeji wa nchi hii pia ingechukua muda mwingi kushughulika na masuala ya mahakama wakati kesi ikiendelea hasa ukizingatia sisi ni wanafunzi . Tulimwomba Mh. A.M.R Mwamanenge atusaidie kutafuta njia ya msingi amabayo itatufanya tuishi kwa amani na kupata msaada wa polisi kwa haraka mara tutoapo taarifa ambazo zinaitaji msaada wao.Watuhumiwa walikukubali kulipa fidia ya kiasi cha 18,000Rupees ambazo vijana hao walitozwa na mwenye nyumba kufidia uharibifu wa mlango.
Tarehe 19/03/2010 nikiwa kama Mwenyekiti wa jumuiya ya waTanzania waishio Bangalore (TASABA) niliongozana na Mh. A.M.R Mwamanenge mpaka ofisi za High Commissioner wa polisi Bangalore na kuonana na Msaidizi wa Commissioner wa polisi Bangalore na kumweleza juu ya suala hilo na hatua zilichokuliwa kwa malengo ya kuzidisha usalama wa waTanzania waishio Bangalore- India, alitupa mikakati ya jinsi watakavyotusaidia kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India. Tulifika pia kwa Inspector General of Police wa Bangalore na kumjulisha pia juu ya suala hili. Hivyo kwa sasa ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na jeshi la polisi watapanga mikakati ya kuhakikisha kuwa amani na haki inatendeka kwa wananchi wa kiTanzania waishio Bagalore- India.

Ushauri wangu kwa waTanzania wale wanaotaka kuja kusoma Bangalore-India katika fani mbalimbali, wakati wanapotuma maombi ya shule au wanapotafuta shule/ vyuo wawasiliane na Mwenyekiti wa jumuiya ya waTanznia waishio Bangalore- India (TASABA) ili wapate msaada wa kimaelezo juu ya vyuo wanavyotafuta. Hii itasaidia kuwaweka waTanzania wasomao huku kwa pamoja na pia kuwatafutia makazi sehemu ambazo hazina fujo na za usalama zaidi kwao ili pale wapatapo matatizo wakiwa wanaishi sehemu moja kwa ukaribu zaidi wapate kusaidiana kwa njia moja au nyingine.Nawasihi pia wale wote waishio Bangalore na kwingine kote nchini India kuzingatia sheria na kanuni za nchi husika na kujiepusha na vyanzo vyote vinavyopelekea fujo kutokea.

kwa niaba ya waTanzania waishio Bangalore na uongozi wa TASABA, tunakushukuru sana Mh. Balozi kwa msaada tulioupata wa kuleta amani baina yetu na wenyeji wa eneo la Hennur Cross, na mikakati iliyowekwa kuhakikisha kuwa tunaishi kwa amani na kupata haki pale tutakapo pata matatizo. Pia namshukuru Mh. A.M.R Mwamanenge kwa kushirikiana nasi bega kwa bega kuhakikisha haki inapatika na kuleta amani na ulewano baina yetu na wenyeji hao na kutujengea nafasi nzuri ya kusikilizwa matatizo yetu mara tufikapo katika kituo cha polisi, ni dhahiri kuwa kwa sasa waTanzania waishio Hennur Cross/ Bangalore wataishi kwa amani. Naomba tuzidi kupata msaada kama huu au zaidi mara kwa mara pale tupatapo matatizo ambayo yatakuwa nje ya uwezo wetu kuyatatua.


Fidelis Msomekela
Mwenyekiti – TASABA
+919742176980

Sunday, March 14, 2010

KUCHOMEWA NYUMBA MOTO KWA WANAFUNZI.

Tarehe 11/03/2010 majira ya saa 10:45 usiku walifika vijana 4 wakidai kuwa wamefanyiwa fujo na Wahindi kwa kurushiwa mawe na kupigiwa kelele za wizi. Vijana hawa walikuwa wanatoka nyumbani kwa wenzao ambako walikuwa wamekutana kupanga jinsi gani watakavyo wakilisha nchi yetu Tanzania katika sherehe ya ‘International Students Day’ itakayofanyika chuoni kwao Indian Academy degree college tarehe 19/03/2010, ndipo walipokuwa wakirudi wakakutana na Wahindi wawili waliokuwa kwenye gari wakiwa wamelewa ambao hupaki gari sehemu karibu na nyumbani kwa wenzao ambao ni; Hamis Mbelwa Fintan mwenye passport No. AB329730 na Olais Alexendra Siarra mwenye passportNo. AB329755waliokuwa wanakaa No.1093/1.11th Cross,Swarnanagar,Robertsonpet,KGF-563 122. Wahindi hao waliwasimamisha vijana hao wakitaka kujua walikuwa wanatoka wapi muda huo wa saa 10:30pm na kama wana vibali vya kuishi nchini, walipogundua kama walikuwa wamelewa waliwapuuza na kuendelea na safari yao, bila kujua kilichokuwa kinawatokea wale wahindi wawili walianza kupiga kelele na baadhi ya majirani kutoka na silaha kama, marungu, nondo na kuanza kuwakimbiza huku wakiwarushia mawe, kwa bahati nzuri hakuna majeruhi. Walipofika kwangu walinielezea kilichotokea nikawasihi wakae kwangu wasitoke mpaka pale hali itakapokuwa shwari. Tukiwa ndani mnamo majira ya saa 11:30pm Olais Alexendra Siarra alinipigia simu kunitaarifu kuwa wale wahindi bado wamekusanyana katika nyumba wanayoishi na wanataka wavunje mlango niliwasihi wasifungue huku nikiwa natafuta jitihada ya kuwasiliana na police, muda si mrefu Hamis Mbelwa Fintan alinipigia simu akinieleza kuwa wale wahindi wamemwaga mafuta ya petrol mlangano kwao na dirishani kisha wakawasha moto, moto ulifanikiwa kuwaka malangoni na kupenya ndani ambako walifanikiwa kuuzima ule wa ndani ukiwa wa nje unaendelea kuwaka. Majirani wanaokaa nyumba moja walitoka na kusaidia kuzima ule wa nje. Bahati nzuri petrol haikua nyingi na hakuna aliyejeruhiwa.

Nilitoka nikatafuta njia ya kufika kituo cha Police cha Hennur Cross, nilitoa taarifa hiyo wakatoka maafisa wa police na kufika sehemu ya tukio wakati huo mimi nikiwa nimebaki kituoni. Baada ya dakika 30 police walirudi bila watuhumiwa, nilpouliza walinijibu nirudi nyumbani wameshawatuliza na hawatarudia tena nilibishana sana na police juu ya hilo maana walipofika waliwakuta watuhumiwa na kuwaachia waende huru. Nilizidi kupigania haki lakini walinijibu “This is India not Tanzania and we have to coup with them like or not” niliwauliza kama huo ndio utamaduni wao wa kumwagia watu petrol na kuchoma moto kutaka kuwaua? Wakasema kama naona hawajanisaidia niende kutafuta msaada mahali pengine. Nilisikitika sana kwa kauli za police hasa ukizingatia kuwa toka Imran Mtui afariki ni mwezi tu na siku 6 mpaka sasa na hatujapata taarifa ya kuridhisha kutoka kwa police halafu linatokea jaribio linguine la kuua kwa kutumia petrol. Mh. Balozi hali hii inanitisha hasa nikiwa kama mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi kuona raia wenzangu wanatishiwa kutolewa maisha yao kwa moto na bila hatia huku police wakiona jambo hilo ni la kawaida kwao na kuwaachia watuhumiwa waende huru. Watu hawa wanaishi nchini kwetu kwa amani na kufaidi matunda ya uhuru na uchumi wa nchi yetu bila bugudha. Naomba ofisi yako teule iingilie kati suala hili leo hii walikuwa na petrol kidogo siku nyingine itakuaje?

Baada ya kuona hakuna masaada niliwashauri Hamis Mbelwa Fintan na Olais Alexendra Siarra wahame mahali pale kwani hapana usalama tena. Tulimtafuta landlord na kuongea nae akakubali kurudisha Deposit yao na kwa sasa wamehama wanaishi na rafiki zao huku wakitafuta nyumba nyingine. Hii ndo hali halisi inayotukuta raia wa Tanzania tusomao huku Bangalore. Ni matumaini yangu kuwa tutapata msaada wa kutosha kutoka ofisi za Ubalozi.

Natangukiza shukrani zangu za dhati,

Fidelis Msomekela

Mwenyekiti - TASABA

Monday, March 8, 2010

TANGAZO

GRADUATION YA TASAA HIPO NJIANI

VYETI VYA VIONGOZI VYATOKA.

YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA TASABA KUHUSU MAANDALIZI YA SHUGHULI YA WAHITIMU.


Siku ya jumamosi uongozi wa TASABA ulikutana na wahitimu ili kuandaa sherehe ya wahitimu ya mwaka 2009-2010 mambo mengi yalizungumziwa ikiwemo na kuandaa kamati kuu itakayo shughulikia shughuli hii.Kamati imefikia maamuzi ya kufanya shughuli hiyo siku ya tarehe 17 aprili 2010 katika ukumbi wa hoteli ya "The club".Mpaka kikao kinaisha kamati ilikua imeshaanza taratibu za kumtafuta mgeni rasmi na kutafuta taarifa na idadi rasmi za wahitimu ili kuwaandalia vyeti na kutengeneza bajeti ya shughuli.Mchango na mawazo ya wahitimu ni muhimu sana kuhusiana na shughuli hii. Kwa michango au mawazo nenda "TASABA group Facebook" au wasiliana na msemaji TASABA (9901837490).

VYETI VYA TASABA VIKO JIKONI TAYARI VYA WASUBIRI WAHITIMU WA MWAKA HUU

Tuesday, March 2, 2010

YALIYOJIRI INTERNATIONAL STUDENTS DAY GARDEN CITY COLLEGE

Wageni wakijaribu kujifunza na kununua vitu mbalimbali toka Tanzania........
Muheshimiwa Rais hakuwepo nyuma alikuwepo kuhakikisha mambo yanaenda sawasawa.......
Mweka hazina nae hakuwa nyuma alipiga vazi la kimasai.................
Tisheti za Hayati baba wa Taifa pia ziliuzwa...................

Dada Hakika ndani ya vazi la kitenge

SHUKRANI TOKA TASABA.

Uongozi wa TASABA chini ya Rais Fidelis Msomekela kupitia wizara ya jamii na utamaduni unatoa shukrani kwa waTanzania waliojitokeza na kuiwakilisha nchi yetu siku ya nchi za kimataifa katika chuo cha Garden City Bangalore.Tunashukuru kwa kulifanya banda letu la wa Tanzania kuwa ndio banda bora pamoja na kutuwakilisha katika kuonyesha mavazi mabalimbali ya asili ya taifa letu.Pia shukrani rasmi zimuendee waziri Mushobozi Baitani kwa kupata cheti baada ya kushinda nafasi ya kwanza kama mchezaji bora wa ngoma ya asili.