Uongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa kiTanzania waishio Bangalore chini ya mwenyekiti Jumanne Mtambalike, unatoa salamu za mwaka mpya kwa watanzania wote waishio India na ulimwengu mzima kwa ujumla.Jumuiya inaitakia seriali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia ubalozi wake India mwaka mpya wenye kheri na fanaka.Uongozi wa TASABA unahamini kwamba huu ni mwaka mpya hivyo basi kwa waTanzania wote nyumbani na ulimwenguni kwa ujumla hatuna budi kujipanga upya kuhakikisha taifa letu linapata maendeleo .Tunaamini kutokana juhudi za wazalendo ndani na nje ya nchi, taifa letu litafanikiwa kuyakabili matatizo mama ya nchi yetu ; ujinga,maradhi na umasikini ulio kithiri.
Tunahimiza wahitimu waliomaliza elimu zao za stashahada za juu maeneo mbalimbali ulimwenguni kurudi nyumbani kwenda kusaidia taifa letu.Mawazo mapya na elimu tuliyoipata vitasaidia kukuza kasi ya maendeleo ya taifa letu.Tuachane na tabia za kung’ang’ania kwenye nchi za watu bila shughuli za msingi wakati taaluma yetu inahitajika nyumbani.Tunayo mifano ya NRI (non- residential Indians) wanavyosaidia nchi yao kukua kiuchumi kwa kuwekeza na kufanya tafiti mabalimbali ndani ya nchi yao japokua wanaishi ugenini.Kama linawezekana kwa wenzetu na sisi pia tunaweza.Hii ni changamoto kwa wahitimu wakiTanzania sehemu yoyote ile ulimwenguni ambao wanahitimu mwaka 2011.Swala la kukaa nje ya nchi na kulaumu mfumo mzima wa utawala na uendeshaji wa nchi yetu halitosaidia lolote kama sisi wenyewe hatuko tayari kuwa chachu ya mabadiliko hayo.
Uongozi wa jumuiya unapenda kukumbusha wazazi na watu mbalimbali wanoleta vijana wao kusoma India kwamba wawe makini na tarehe za kufanya usajili wa wanafunzi kwenye vyuo mbalimbali.Mwaka jana tumekumbwa na tatizo la vijana wengi wa mwaka wa kwanza kukosa namba zao za mitihani kutokana na kuchelewa kuhudhuria vyuoni.Tatizo hili linazaa tatizo jingine kubwa ambalo ni vijana kukaa Bangalore bila shughuli za msingi hali ambayo ni hatari sana kwani mtu anakua ana viza ya mwanafunzi halafu shule haendi kutokana nakuchelewa usajili.Hali ambayo inatuweka sisi viongozi katika wakati mgumu kumsaidia huyo mtu akipata matatizo.
Uongozi unakumbusha wanajumuiya kwamba usajili wa majina yao kwa ajili ya kuyapeleka ubalozini mwisho ni tarehe 30 Januari.Uongozi unasisitiza watu kujisajiri na kuhakikisha wanapata vitambulisho vya usajili ili wapate msaada pale unapohitajika.Itasaidia pia kuweza kuwatofautisha na waafrika wengine waishio India kama kutatokea tatizo.
Tangazo la mwisho wahitimu wote wanaohitimu mwaka 2011 watume majina yao , kozi zao na vyuo wanavyosoma kwa uongozi wa TASABA kabla ya mwezi machi kwa ajili ya maandalizi ya siku ya kuhitimu.Zoezi hili lifanywe haraka hiwezekanavyo kwa ajili ya utengenezaji wa vyeti vya jumuiya.
Mungu ibariki jumuiya yetu pamoja na taifa letu kwa ujumla.
Rais TASABA: Jumanne Rajabu Mtambalike
0 comments:
Post a Comment