TANZANIA STUDENTS ASSOCIATION BANGALORE
(TASABA)
14/12/09
Salamu kwenu nyote,
Ndugu wa Tanzania wenzangu napenda kuchukua nafasi hii kuwa kumbusha juu ya swala la kujiandikisha kuwa mwanachama hai wa TASABA. Fomu zote na maelekezo wanayo viongozi wote wa vitongoji. Ni muhimu sana kujiandikisha kwani tunahitaji kujua hapa Bangalore kuna wa Tanzania wangapi pia tuweze kutengeneza vitambulisho ambavyo ni muhimu sana kuwa navyo.
Pia napenda kuwasisitiza kuwa wale wote wenye matatizo ya R.P (Residential Permit) na VISA tafadhali julisha uongozi wa TASABA ili tuweze kuwasaidia mapema kabla mambo hayajawa magumu zaidi.. Pia ni muhimu sana kuzingatia sheria na kanuni zote za uhamiaji ili kuepuka matatizo kama hayo. Wengi wenu mmeshashudia baadhi ya wenzetu wanavyopata matatizo makubwa juu ya mambo hayo.
Ndugu wa Tanzania wenzangu tukumbe mila na utamaduni wetu ni Amani, Umoja na Mshikamano. Nawaomba sana tudumishe utamaduni wetu kwa kuishi kwa amani baina yetu na wenyeji wan nchi hii. Masuala ya ugomvi kati yetu sisi kwa sisi au na wenyeji wetu hayatujengi zaidi ya kutupa sifa mbaya ambayo hapo baadae itatufanya tuishi katika wakati mgumu na inaweza kuwapa wakati mgumu wenzetu watakao kuwa wanahitaji kuja kusoma India siku zijazo. Naomba tufanye starehe za kiasi na za Amani. Tunaelekea kufunga mwaka kwa wale wote tuliobaki hapa Bangalore katika likizo hii naomba sana tuitumie vyema na ninategemea kuwa sitapata malalamiko ya ugomvi au tabia zozote zile amabzo si nzuri toka kwa jamii tunayoishi. Tukumbuke huku tuko ugenini na ni mbali na nyumbani hivyo tatizo lolote utakalolipata litasumbua mpaka wazazi nyumbani ambao wana kazi nyingi za kufanya .
Napenda kuwakumbusha tena kwa wale wote tunaotumia vyombo vya usafiri binafsi hasa pikipiki naomba tuwe makini sana. Najua kuna msemo usemao “AJALI HAINA KINGA” lakini tusichukulie msemo huu kama kigezo najua kuna ajali nyingine zinasababishwa na sisi wenyewe ama kwa kujiamini kuwa ni madereva wazuri au kwa kupenda sifa kutoka kwa wenzetu au kwa kushindwa kumiliki vyombo hivyo kutokana na ulevi. Tuna mifano mingi kutoka kwa wenzetu waliopata ajali hivyo basi nawaomba tuwe makini sana ili kuepuka tatizo hili najua wote ni watu wazima hivyo mtalizingatia hili kwa undani zaidi.
ndugu wa Tanzania wenzangu nazidi kuwaomba kutoa michango yenu ya halina Mali katika chama chetu ili kukijenga kiwe imara zaidi na cha manufaa kwa jamii nzima. Tukumbuke kuwa chama hiki ni chetu sote na kila mwanajumuiya ana haki sawa juu ya chama hiki katika kukijenga na kuleta maendeleo. Jukumu hili ni letu sote na si la viongozi wa chama au kundi Fulani. Napenda kuwa hakikishia kuwa TASABA hakifungani na kundi lolote lile kama uvumi uliopo. Uongozi wa TASABA ni uongozi wa jumuiya nzima na hauna kundi na wala hautakuja kuwa na kundi. Uongozi wa TASABA una wajibu wa kushirikiana na kila mwanajumuiya katika shida na raha hivyo basi hata siku moja hauta kuwa na manufaa katika kundi Fulani au mtu mojamoja uongozi huu ni wa kila mTanzania. Naomba tusiwe na mawzo potofu pia kuwakemea wale wote ambao wana mawazo potofu kama haya juu ya TASABA, kauli mbiu yetu ni “UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU” tushirikiane kwa pamoja na kudumisha amani, umoja na heshima miongoni mwetu na kwa jamii tunayoishi.
Napenda pia kuchukua fursa hii kuwapa pole wale wote waliofiwa na wazazi, na ndugu, kwa kipindi hiki. Mwenyezi Mungu awepe moyo wa uvumilivu na kuwaongoza vyema katika wakati huu mgumu mlikokuwa nao. Pia natoa pole kwa wale wote milopata matatizo ya kijamii, ugonjwa na ajali. TASABA ipo pamoja nanyi na itanedelea kushirikina nanyi bega kwa bega.
Nawatakia mapumziko mema, Mwenyezi Mungu awatangulie, awape afya njema, Hekima, Busara,Maarifa na mafanikio katika masomo yenu.
FIDELIS MARTINE MSOMEKELA
RAIS - TASABA
0 comments:
Post a Comment