Tuesday, December 8, 2009
YALIYOJIRI SEMINAR YA NOKIA FORUM 2010
Jana tarehe 7 decemba 2009 katika hoteli ya Taj Residency Mahtma Gandhi road hapa Bangalore,kulikua na semina kubwa ya watengenezaji wa simu wakubwa duniani wa kampuni ya Nokia baadhi ya wanafunzi wa kitanzania walipata bahati ya kuhudhuria semina hiyo wakiongozwa na msemaji mkuu wa Tasaba Mh.Jumanne Rajabu Mtambalike.
Mambo mengi yalizungumzwa kwenye semina hiyo, hasa katika ulimwengu wa sayansi na tekinolojia mabadiliko mbalimbali ya technolojia za matumizi ya simu zilizungumziwa na namna gani zitaweza kukuza uchumi wa nchi mbalimbali duniani. Semina ilifana na baadhi ya watu walipata fursa ya kujishindia Nokia N-97 pamoja na vitu mbalimbali vilitolewa na kampuni ya Nokia vikiwemo simu kwa washindi mbalimbali na kwa walihoudhuria walipata mabegi ya laptop,CD za software za mafundi wa nokia,pamoja na CD za graphics za kampuni ya Adobe Photoshop CS4,t-shirt,key olders na vitu vingine vingi ikiwa pamoja na kutambulika kama ni maofisa wapya wa Nokia duniani.
Mh Jumanne akilizungumzia hilo amesema hii ni changamoto kwa wanafunzi wote wakitanzania kujihusisha katika mambo kama haya kwa ajili ya kutengeneza msingi mzuri wa taaluma zao mbalimbali wanazosomea na kusisitiza hii ni nafasi wanayopata wanafunzi wanaosoma nje ya nchi hivyo waitumie vizuri.
0 comments:
Post a Comment