Ads 468x60px

Pages

Monday, October 18, 2010

Mechi ya Kirafiki ya majaribio. (Tanzania vs Nigeria )

Mnamo tarehe 16-10-2010 timu yetu kabambe ya mpira wa miguu ilianza vizuri msimu wake wa mechi za majaribio kwa ajili ya kujiandaa na michuoano mikuubwa ya wanafunzi wageni walioko bangalore (Bangalore's International Students' Annual Sports Tournament ) mnamo mwezi wa kumi na mbili baada ya mitihani ya muhula kwa ushindi maridaaaadi wa mabao mawili kwa moja la kubahatisha la waNIGERIA walioko bangalore.

Huu ni mwanzo tu na uongozi unapenda kuwapongeza wachezaji pamoja na woote walioshiriki katika ushindi huu maridadi na kufanya timu yetu izidi kuogopewa na timu nyingi.

Pia Uongozi unapenda kuwashukuru WaTANZANIA woote waliojitokeza uwanjani kuishangilia timu yote kwa uzalendo mkuubwa hadi kuchangia timu yetu kupata ushindi huo ambao ulikua mgumu kufuatia kwa waNIGERIA hao kubahatisha kagoli kao wakati sie WATANZANIA tukiusoma mchezo.

Tunawasisitiza WATANZANIA tuzidi ishi kwa umoja,amani na upendo na pia wachezaji kuzidi jituma kwenye mazoezi ili michuano ya mwezi wa kumi na mbili tuwe moto wa kuotea mbali kama kawaida yetu kwani nguvu tunazo,nia tunayo na uwezo hasa wa kushinda michuano hiyo tunao.

Mungu ibariki TASABA,
Mungu Ibariki Tanzania...

Wizara ya Michezo

0 comments:

Post a Comment