Ads 468x60px

Pages

Monday, October 18, 2010

Mechi ya pili ya kirafiki(Tanzania vs Sudan)

Katika kujaribu kuzidi jenga undugu,upendo na ushirikiano na jamii zingine za wanafunzi mbalimbali watokao nchi zingine hapa Bangalore, TASABA chini ya wizara yake ya michezo ilijaribu weka mechi nyingine ya kirafiki mnamo tarehe 17-10-2010 siku ya jumapili kwa ajili pia ya kujipima nguvu na kuifua timu yetu.

Lakini kutokana na sababu zilizokuw anje ya uwezo wetu,pamoja na wachezaji na washabiki mbali mbali kufika uwanjani kushangilia nchi zao,mechi hiyo ilibidi na kulazimika kuahirishwa mpaka hapo itakapotangazwa hapo baadae.

TASABA inajaribu kufanya kila liwezekanalo ili mechi hiyo iweze chezwa mapema kabla wachezaji hawajapewa mapumziko maalumu kwa ajili ya kuwawezesha kujiandaa vyema na mitihani yao ya kumaliza mwaka wa masomo.

Tunawashukuru WaTanzania woote waliojitokeza na twawaombeni tuzidi kuwa na moyo huo huo.

Mungu ibariki TASABA,
Mungu ibariki Tanzania...

Wizara ya michezo

0 comments:

Post a Comment