Vikao bado vinaendelea na ajenda kuu ni kujadiliana juu ya budget ya Tanzania kwa mwaka wa fedha wa 2011 - 2012 na kuipitsha.
Waziri wa Fedha Mh. Mustapha Mkullo akiwasili bungeni kusoma budget ya 2011 - 2012
Waheshmiwa wabunge pamoja na waziri mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda wakiteta mambo mawili matatu.
Mheshimiwa Mbunge Edward Lowassa akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha upinzani cha APPT maendeleo ndugu Peter Mziray
Waziri wa Katiba, Mheshimiwa Celina Kombani akiteta jambo na mheshimiwa mbunge kijana aliyegraduate mwaka jana pale UDSM..Mheshimiwa David Kafulila wa jimbo la Kigoma Kusini
Waheshimiwa wabunge A. Lyatonga Mrema (katikati ) na Stephen Ngonyani maarufu kama Profesa Maji marefu (kushoto ) wakiteta jambo na naibu waziri wa fedha mheshimiwa G. Teu
0 comments:
Post a Comment