Ads 468x60px

Pages

Sunday, February 27, 2011

MSIMAMO WA MAKUNDI YETU HADI TWAINGIA MITAMBONI


KUNDI A
TEAM P W D L GF GA PTS
TEAM SUDAN 3 2 1 0 8 0 7

,'CAMEROON 3 2 0 1 3 1 6

,.'. RWANDA 3 1 0 2 2 3 4

.'. UGANDA 3 0 0 3 1 10 0


KUNDI B

TIMU P W D L GF GA PTS

TEAM NIGERIA 3 3 0 0 7 2 9

~.'. TANZANIA 3 1 1 1 4 2 4

' IVORY COAST 3 1 1 1 3 3 4

TEAM CONGO 3 0 0 3 0 8 0



NB:
P = Matches Played
W = Matches won
D = Matches drawn
L = Matches Lost
GF = Goals for
GA = Goals against
Pts = Points

* Top two teams from each group qualified to the semi finals stage..

Sudan are the winners of Group A and Cameroon are the Runners up of Group A...

Nigeria are the winners of Group B and Tanzania are the Runners up of Group B...


Habari na picha zaidi za mashindano yetu haya zitawajia muda si mrefu…

MATOKEO YA MECHI ZA MASHINDANO SIKU YA JUMAPILI


Cameroon 1 - 0 Uganda

*Tanzania 3 - 0 Congo

*Nigeria 3 - 0 Ivory Coast

Sudan 7 - 0 Uganda

Tanzania 1 - 2 Nigeria

Rwanda 0 - 2 Cameroon


Magoli yaliyopatikana siku ya pili ya masindano ni magoli 19
na hivyo kufikisha jumla ya magoli 27.

Mechi zote leo zilikua za ushindi zikiwemo mbili za ushindi wa mezani

* = Timu ilipewa ushindi wa mezani wa magoli matatu kwa bila mara baada ya timu pinzani kukiuka baadhi ya kanuni na masharti ya ya mashindano.

MATOKEO YA MECHI ZA MASHINDANO YETU SIKU YA JUMAMOSI


Nigeria 2 - 1 Congo

Uganda 0 - 1 Rwanda

Tanzania 0 - 0 Ivory Coast

Sudan 1 - 0 Cameroon

Congo 0 - 3 Ivory Coast

Rwanda 0 - 0 Sudan

Kwa siku ya kwanza, jumla ya magoli 8 yalipatikana katika mechi 6

Ambapo draw mechi zilikua 2 na za ushindi zilikua 6


Twawatakia heri katika mechi zilizobakia timu zote hasa timu yetu Tanzania itutoe kimasomaso

Thursday, February 24, 2011

Soccer Tournament


It's Time for Africa people.......
Ladies and Gentleman, its now time for us "Afircans" in Bangalore to come together and enjoy a football tournament which will be taking place in CHRIST UNIVERSITY, KORAMANGALA on 26th and 27th february with 12 Group stage matches involving 8 teams and semi finals would be held on 5th March evening, and 3rd position and final match would be held on 6th March, 2011.

Teams which have confirmed as of now are Cameroon, Congo, Ivory coast, Nigeria, Rwanda, Sudan, Tanzania and Uganda.

Lets all come together and enjoy the tournament in a friendly manner!!!!

Wednesday, February 23, 2011

MAZOEZI YA TIMU YETU YAENDELEA VYEMA


Viongozi wa TASABA wakiwa pamoja na viongozi wetu wa timu bwana Jerome na Big Willy mara baada ya mazoezi ya timu.

Wachezaji wakiwa hoi wakijadiliana mawili matatu mara baada ya mazoezi yao




makapteni wakiwa pamoja na mkuu wa nidhamu






Wa Tanzania walijitokeza kwa wingi pia kutazama mazoezi ya timu yao na kuipa moyo kuanzia mwanzoni.

Timu yetu ya Tanzania yaendelea vyema na mazoezi yake kujiandaa na mashindano ya "TASABA CUP OF AFRICAN NATIONS" ambapo jana kwa mara ya kwanza wa Tanzania wote walioko Bangalore kutoka kona zote za bangalore walikutana viwanja vya Banaswadi na kufanya mazoezi babu kubwa kama ionekanavyo kwenye picha mbali mbali.

Wapinzani wetu wakae mkao wa kuja kufungwa tu, lazima wapoteane uwanjani.

Mungu ibariki timu yetu.


NB: UONGOZI WA TASABA UNAWASHUKURU WACHEZAJI WOTE KWA MOYO WAO WA KUJITOLEA NA UNATUKANA NA TIMU NZIMA PAMOJA NA UONGOZI YAKE SIKU YA IJUMAA VIWANJA VYA BANASWADI KAMA UONGOZI ULIVYOPENDEKEZA

Monday, February 21, 2011

MAKABIDHIANO YA VIFAA NA KIKAO CHA MWISHO NA MAKAPTENI WA NCHI ZOTE..


Mwenyekiti wa U.A.C.B bwana Jimmy akionyesha mfano wa jezi mojawapo jinsi zilivyoandikwa kwa mbele na kwa nyuma zitakua zimeandikwa jina la nchi.


Ndugu Khalidi naye akaona ni vyema walau aone quality ya jezi zetu na kuziwekea Baraka zilete ushindi tu


Hawa ndio hawawezi kukosa na ndio vibonde wetu tutakao fungua nao dimba siku ya jumamosi, kwa jinsi tukijuavyo kikosi chetu maridadi, lazima wa Ivory Coast watukome siku hiyo Uwanjani CHENGA WATAZILA na MABAO vile vile nayo WATAYALA tu WAPENDE WASIPENDE!!!
Macaptain wa timu zingine kama Uganda, Nigeria, Congo na Cameroon wakifuatilia kikao


Macaptain wa timu zingine kama Uganda, Nigeria, Congo na Cameroon wakifuatilia kikao


Mkuu wa Nidhamu wa timu yetu ya WA TANZANIA na mweka Hadhina wa U.A.C. B ndugu William akifuatilia kwa umakini mkubwa muendelezo wa kikao hicho pamoja na wawakilishi kutoka nchi zingine.



Nigeria nao wakaja


Congo wakafuatia


Haya sasa timu na uongozi mzima wa timu, mtake na kupewa nini tenaaaa?vifaa ndio hivyoo vimepatikana, sie waTanzania twataka MTUPE RAHA TUU!!!

Mungu ibariki TASABA,
Mungu ibariki TANZANIA...

MAKABIDHIANO YA JERSEY NA VIFAA MUHIMU VYA TIMU ZOTE YAFANYIKA


Katika maandalizi ya Mashindano ya Nchi za KiAfrika hapa Bangalore yaendeleayo, Uongozi mzima wa TASABA ulisimama kidete kuhakikisha timu zote zapewa vifaa vyao muhimu kwa ajili ya mashindano hayo walau week moja kabla ya mashindano kuanza na hivyo ndivyo ilivyofanyika.

Wadhamini wakuu wa mashindano haya jana walihudhuria kikao kilichoitishwa na ungozi na macaptain na timu zote shiriki na kuweza someana sheria za mashindano, ratiba ya mashindano na pia kukabidhiana vifaa vyote muhimu, ambapo timu zoote zilipewa jezi ya kaptula, ya juu na soksi pamoja na kitambaa cha kapteni kwa kila timu, kitu kilichokua mojawapo ya makubaliano ya uongozi wa TASABA na Union of African Communities.

Tunaomba kusisitiza ieleweke kuwa TASABA ndio main Organizers wa Mashindano haya, na Union of African Communities in Bangalore ni wadhamini tu.
Tunapenda itakia timu yetu kila la kheri katika maandalizi ya mashindano hayo, wafike fainali na kuhakikisha kikombe kinabaki TASABA na wawafurahishe wa Tanzania nasi Uongozi tutajitahidi kuwa nao bega kwa bega.

Vifaa hivyo vya michezo viko chini ya Uongozi wa TASABA na uongozi wa timu chini ya Meneja Jerome na mkuu wa nidhamu Big Willy watakabidhiwa vifaa hivyo jhivi karibuni. Na mara baada ya mashindano hayo vifaa hivyo VITAPASWA KURUDISHWA NDANI YA HIMAYA YA UONGOZI WA TASABA, havitakua mali za watu binafsi kila mchezaji kuondoka nazo.

TUSHIRIKIANE PAMOJA KULETA KOMBE HILI NYUMBANI.

TUIPE SUPPORT TIMU YETU YA TANZANIA

Uongozi wa TASABA unawaomba wa Tanzania woote wasomao na kuishi Bangalore kujitokeza kwa idadi kubwa kuja ipa support, kuitia moyo na kuishangilia timu yetu pindi itakapokua inacheza mechi zake mbali mbali ili kusaidia nchi yetu kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Tunaombwa kujitokeza kwa wingi kwani kutakua na usafiri wa kwenda viwanjani Christ University, Koramangala na wa kurudi katika pick up point mtakazo kuwa mnachukuliwa mara baada ya nyie kutuhakikishia uwepo wenu.

Pia tunawaomba wale waishio karibu na maeneo ya viwanja hivyo kujitokeza kwa wingi uwanjani pasipo kusubiria usafiri au kusukumwa na UONGOZI, na kwa wale wenye kujisikia kuisaidia timu yetu kwa namna moja au nyingine ikiwemo ya michango mbalimbali ya vifaa,dawa,fedha au hata ya kimawazo tunawakaribisha sana, milango I wazi kuwasikilizeni na kushirikiana nanyi.

Tunawaomba wachezaji wetu nao wafanye mazoezi kwa bidii ili waipeperushe vyema bendera yetu ya Tanzania.
Hizi ni mechi za Tanzania kwa siku ya jumamosi na jumapili Christ university.

Jumamosi tarehe 26, saa tano unusu asubuhi, Tanzania itakipiga na Ivory Coast

Jumapili tarehe 27, saa nne asubuhi, Tanzania itapambana vilivyo na Congo

Jumapili tarehe 27, (siku hiyo hiyo) ila saa nane mchana, Tanzania itamaliza dimba na Nigeria.

Ndugu wa TANZANIA, tusikose mechi hizi nzuri na za kuvutia kwani ndio wasaa wetu kujumuika pamoja na kujivunia UTanzania wetu, tusiwe tu twakutana sehemu za starehe na misibani.

Mungu ibariki TASABA,
Mungu ibariki TANZANIA…

MASHUJAA WETU TOKA GARDEN CITY COLLEGE


hawa watatu ndio mashujaa wetu toka garden city college ambao timu yao iliweza ibuka kidedea katika mashindano ya mpira wa miguu ya FISA-B, bwana Kainkwa Luseko, Abuu na Uthman Yunus ambapo Abuu alifunga goli la mwisho la mashindano hayo.
Katika Picha hii wakiwa pamoja na Mweka Hadhina wetu ndugu Vince Nkini mara baada ya kukabidhiwa vikombe na zawadi zao za ushindi

MATUKIO YA MECHI YA FAINALI YA FISA-B KATIKA PICHA


Uongozi Mzima wa Fisa-B ukiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya makabidhiano ya zawadi za washindi mara tu mechi ya fainali ilipoisha.


Washindi wa tournament ya international students ya Fisa-B wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa kikombe chao,medali,vyeti na zawadi mbali mbali.


Mchezaji bora wa Tournament nzima toka Garden City College, Ahmed toka Sudan akipokea zawadi zake pamoja na kikombe cha ushindi.


Mfungaji bora wa Tournament nzima toka Garden City College, Bakari toka Ivory Coast akipokea zawadi zake.


Captain wa timu ya Christ University na Rais wa Fisa- B, Ndugu Antonio toka Mozambique akipokea cheti chake na zawadi toka kwa mgeni rasmi huku viongozi wengine wa Fisa- B wakishuhudia.


Captain msaidizi wa timu ya Garden City College toka Tanzania ndugu Kainkwa akiongoza mazoezi ya viungo ya timu yake kabla ya mechi huku wachezaji wengine wa kitanzania ndugu Uthman ( # 3) na ndugu Abuu (# 6) wakipasha viungo moto tayari kwa mechi yao ya fainali

FISA-B’s FOOTBALL TOURNAMENT YAMALIZIKA VYEMA

Mashindano ya mpira wa miguu ya The Federation of International Students Association in Bangalore yaliyokuwa yameandaliwa ki vyuo yalifikia kilele chake jana kwa mechi ya kuvutia ya fainali iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Christ, Koramangala baina ya timu za Christ University na Garden City College.

Mechi hiyo ilikua ya vuta ni kuvute ambapo hadi kipindi cha kwanza kinaisha, GCC walikua wanaongoza kwa goli moja lakinii Mpaka Refarii anapuliza Kipenga cha mwisho GCC walikua wana magoli manne huku Christ University wakiwa hawajajibu hata moja.

Tanzania ilipata bahati ya kuwakilishwa na WaTanzania watatu wasomao chuo cha GCC katika mechi hiyo ya fainali ndugu Kainkwa, Abuu na Uthman na pia Uongozi mzima TASABA uliwakilishwa vyema na wawakilishi wake wa TASABA ( Ndugu Hartman, bi Mariam, bi Mwamini, bi Magdalena na bi Eunice J) pamoja na Makamu wa Rais (Anase) na Mweka Hadhina (Vince) mara baada ya kupata mwaliko toka FISA-B, huku Rais na Katibu wa TASABA wakihudhuria vikao vingine.

Uongozi unapenda wapongeza GCC kwa ushindi wao hasa WATANZANIA wale watatu kwa kuipeperusha vyema bendera yetu, na sasa tuelekeze nguvu zetu zoote kuipa moyo timu yetu ya Tanzania kwenye tournament yetu itarajiwayo kuanza jumamosi.

Mungu Ibariki TASABA,
Mungu ibariki TANZANIA..

Saturday, February 19, 2011

GRADUATION ANNOUNCEMENT.

On the meeting held on 19th Feb 2011 between the graduates and TASABA leaders we have decided the graduation to be on 2nd April 2011.The agreed venue is COUNTRY CLUB. Each graduate should pay 1700rupees before 15th March. Please spread this massage to others.End anyone wishing to attend the graduation party should pay 500rps except guests of honor.

Thursday, February 17, 2011

BREAKING NEWS: MABOMU GONGO LA MBOTO

Ndugu watanzania, tunapenda kuwataarifu kuwa MABOMU yanalipuka kwenye army airport base, Dar es salaam.
Tunaomba muwasiliane na familia zenu.
UONGOZI - TASABA.

WATU WATAKIWA NA KUWA WATULIVU NA KUHAMA MAENEO YA GONGO LA MBOTO NA TABATA NA KUKAA MAENEO YA WAZI


Mnadhimu mkuu wa majeshi, Tanzania Luteni Jenerali ABDURAHAMAN SHIMBO amewataka na kuwasihi waTanzania kuwa watulivu na kutulia katika maeneo yaliyo ya wazi ili kuwa katika hali ya usalama zaidi.
Pia, watu wanaoishi karibia na kambi za jeshi kuondoka katika maeneo hayo ili kuwa katika hali ya kiusalama zaidi.
Mpaka sasa hivi chanzo cha ulipukaji wa mabomu hayo yaliyoleta milio na vishindo katika jiji la Dar es salaam bado haujajulikana ila uchunguzi bado unaendelea.

UONGOZI TASABA..

ULIPUKAJI WA MABOMU DAR ES SALAAM




Uongozi wa TASABA unasikitika kuwataarifu ya kuwa kuna habari za kusikitisha za ulipukaji wa mabomu katika army base ya gongo la mboto, Dar es salaam..
Tunawaombeni muwasiliane na watu wenu wa karibu nyumbani ili kujua hali ya usalama wa familia,ndugu na jamaa zenu nyumbani Tanzania na pia tuwe watulivu na kuzidisha umoja na kuiombea nchi yetu, hasa katika kipindi hiki kigumu..

Mungu ibariki TASABA..
Mungu ibariki Tanzania..
Mungu ibariki Africa..

Tuesday, February 15, 2011

UTOAJI WA MAONI KATIKA BLOG YETU

Ewe Mtanzania mwenzetu
Kama una maoni ,ushauri,mawazo kuhusu TASABA
tunafurahia na kuthamini mchango wako,
ila tunapenda kusisitiza matumizi ya lugha nzuri,
isiyo na matusi,vitisho,majungu na fitna
kwani haijengi ila inaleta uharibifu wa jumuiya yetu.
Hivyo,tunawaomba sana kutumia hekima na busara kama wasomi
PAMOJA TUTAIJENGA NA KUIMARISHA TASABA YETU!

Monday, February 14, 2011

Tanzanian student dies in road accident

HYDERABAD: A college student hailing from Tanzania died in a road accident near Ghatkesar on Sunday night.

The victim, Nickson Elinwema, 20, was a B Com Ist year student of R K Degree College in Himayatnagar. He came to India in 2010 on a student visa and was living in a flat in Nacharam.

According to Ghatkesar police, Nickson along with his friends consumed alcohol at a bar in Sainikpuri on Saturday night. Nickson then accompanied his friends to their flat in Ramanthapur. At about 1.30 am, without waking up his friends, Nickson got up and took out a scooter to return home.

At Uppal crossroads, Nickson lost his way and called his friends. "They told him that they would come to the spot and asked him not to leave. But Nickson took a U-turn towards Uppal at Narapally and lost control over the vehicle and rammed it into a road divider," Ghatkesar SI R Ravi said.
His friends reached the spot and with the help of police rushed Nickson, who suffered head injuries to Gandhi Hospital, where he was declared brought dead.

Source: Times of India



Tuesday, February 8, 2011

TANBANG


coming soon.........

SHUKRANI ZA UONGOZI WA TASABA‏

UONGOZI WA TASABA unapenda kuwashukuru wooote waliouhusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha uwakilishi wa Nchi yetu ya TANZANIA kwenye shughuli nzima ya FISA-B iliyofanyika Mount Carmel College.

UONGOZI umeguswa na kufurahishwa saana na moyo wa kujitolea ulionyeshwa na baadhi ya WATANZANIA siku hiyo na unaahidi utatafuta njia nzuri zaidi ya Kuwashukuru na Kuappreciate kwa kazi yao nzuri sana siku za usoni.

Pia Uongozi unapenda kuwashukuru Watanzania woote kwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo na unapenda wasisitizia zidisha moyo wa umoja na upendo kwani UMOJA NI NGUVU, na UTENGANO NI UDHAIFU..

Kwa niaba ya WATANZANIA wote tunapenda washukuru

1. Ndugu Eliud Mwanuzi na Abuu toka Garden City College kwa Break Dance yao,wazee na kundi lenu mlitisha vibaya
2. Dada Riian kwa Belly dance na Ushakira if not U Ray C wake,dada kipaji unacho.
3. Dada Eunice Jacob, Magdalena Henry, Sarah Kasango, Mariam Sigera, Neema Witts na Ellen Buhiye kwa performance yao ya mwisho iliyoacha gumzo pia.
4. Ndugu Job Witts kwa kutoa nyumba yake kuwa sehemu ya kufanyia mazoezi kwa zaidi ya week mbili na kufanikisha suala zima la usafiri kwa wengi wa wawakilishi wetu siku hiyo.
5. Viongozi wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha shughuli hiyo siku.

Mungu ibariki TASABA...
Mungu ibariki TANZANIA...

INTERNATIONAL STUDENTS CULTURAL NIGHT IN BANGALORE‏

Baadhi ya Watanzania waliokuwemo kwenye shughuli hiyo Rais Jumanne akiwa na viongozi wastaafu ndugu Ntemasanja pamoja na marais wastaafu Fidelis Msomekela na Baraka KangeWawakilishi wetu wa usiku huo wakiwa na mpiga picha wetu wa usiku huo
Wadada wetu wakiangusha sebene la kufa mtu stejini lilifunika show nziima








Monday, February 7, 2011

Fisa - B International Students Cultural Day‏

Congo Brazzaville akianza imba Opera yake, naye alifunika vibaya mnoo
Ivory Coast wakianza dance yao kwa mkwara mziito
Rwanda wakicheza ngoma yao ya asili
Congo wakilimwaga sebene la kufa mtu
Wanafunzi kutoka garden city college,wakibreak dance ambapo kundi hilo lina watanzania wawili
South Africa wakiangusha kwaito mwanana ndani ya steji

Baadhi ya watanzania waliokuwemo kwenye event hiyo