Ads 468x60px

Pages

Tuesday, February 8, 2011

SHUKRANI ZA UONGOZI WA TASABA‏

UONGOZI WA TASABA unapenda kuwashukuru wooote waliouhusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha uwakilishi wa Nchi yetu ya TANZANIA kwenye shughuli nzima ya FISA-B iliyofanyika Mount Carmel College.

UONGOZI umeguswa na kufurahishwa saana na moyo wa kujitolea ulionyeshwa na baadhi ya WATANZANIA siku hiyo na unaahidi utatafuta njia nzuri zaidi ya Kuwashukuru na Kuappreciate kwa kazi yao nzuri sana siku za usoni.

Pia Uongozi unapenda kuwashukuru Watanzania woote kwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo na unapenda wasisitizia zidisha moyo wa umoja na upendo kwani UMOJA NI NGUVU, na UTENGANO NI UDHAIFU..

Kwa niaba ya WATANZANIA wote tunapenda washukuru

1. Ndugu Eliud Mwanuzi na Abuu toka Garden City College kwa Break Dance yao,wazee na kundi lenu mlitisha vibaya
2. Dada Riian kwa Belly dance na Ushakira if not U Ray C wake,dada kipaji unacho.
3. Dada Eunice Jacob, Magdalena Henry, Sarah Kasango, Mariam Sigera, Neema Witts na Ellen Buhiye kwa performance yao ya mwisho iliyoacha gumzo pia.
4. Ndugu Job Witts kwa kutoa nyumba yake kuwa sehemu ya kufanyia mazoezi kwa zaidi ya week mbili na kufanikisha suala zima la usafiri kwa wengi wa wawakilishi wetu siku hiyo.
5. Viongozi wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha shughuli hiyo siku.

Mungu ibariki TASABA...
Mungu ibariki TANZANIA...

8 comments:

Anonymous said...

Tasaba acheni ubabaishaji na uongo ndani yenu,yani mnatudanganya ndugu yenu job witts amefanikisha swala la usafiri wakati tulimuona ameshuka na familia yake peke yake acheni kupamba watu kisa mnajuana nao au ni marafiki zenu kwa maslahi yenu binafsi..Wekeni undugu na urafiki pembeni mnaboa bwana kwa kujichagua ndo maana hatutaki kushiriki mambo yenu ya kindugundugu.Fisa-B imefanikiwa kwa sababu wana ushirikiano na hawabaguani ndo maana wanaendelea but Tasaba itaishia kupaishana majina tu kwa mambo yasiokua ya muhimu....MNAKERA JIREKEBISHENI TASABA

Anonymous said...

HEEEEEHHHEHE WAPE HAO NATAMANI NIKUJUE NIKUBEBE WAMEZIDI UNDUGULIZATION.

Anonymous said...

Acheni ufala nyinyi na tabia zenu za ku hate watu bila sababu za msingi wakati tasaba inatangaza kushiriki mlijitokeza ? ndio maana wabongo hamna maendeleo website ishatoka ,gazeti lipo njiani na tarehe 27 kuna tournament mkitaka kuja njoeni msipottakka kaeni nyumbani kama kawa speed mia haters imekula kwenu..................

Anonymous said...

bila shaka umejiona mpumbavu kwa kutoweza kuandika jina lako hapo..maana huna ushirikiano wowote. walipotangaza kushiriki ulijitokeza?
na wewe utamaniye kubeba upuuzi,...una matatizo makubwa..
TASABA itadumu,,,wewe hutadumu...wala hakuna atakaye kutambua....
...acha ku hate....

Anonymous said...

sasa wewe bwege mwenye wivu usio na maendeleo,next time toa familia yako na gari lako kwa shughuli za kichama ili nawe usifiwe na ushukurirwe ehh? Utakufa na kijiba chako cha roho na tasaba ipoooo ilikwepo na itakwepoooo

Anonymous said...

loooooh,watu wengine wana wivuuuuuu..
Haya nawe jitaje jinalo basi ili viongozi wakupaishe kama hicho ndicho haswaaa wakitaka.
Halafu waweza kuta huyo ni jianaume ambalo lategemewa lije kuwa baba wa familia yake,lakini akili yake imejaa usaha hadi ikampeleka atoe comment za kipuuzi kama hivyo.
Viongozi endeleeni na moyo wenu wa kujitolea.
Tasaba oyeeeee

Anonymous said...

VIONGOZI WA TASABA mmepewa dhamana ya kuongoza waTanzania wa huko Bangalore kupitia sanduku la kura, msikatishwe tamaa na wapuuzi wachache,wabaguzi wachache wendawazimu wawili watatu... nafikia kuwaita mabaradhuli.
dumisheni umoja wa waTanzania Bangalore
idumu Tasaba!

Anonymous said...

TASABA ipo kwa ajili ya watanzania lkn nyie watu mkialikwa au mkiombwa muje kutoa michango yenu huwa mnajificha, kabla hujahate jiulize umefanya nini cha maana???namba za sim zipo hapo juu za viongozi kama vp we piga sim uelezee matatizo yako wacha longo longo...

Post a Comment