Monday, February 21, 2011
MAKABIDHIANO YA JERSEY NA VIFAA MUHIMU VYA TIMU ZOTE YAFANYIKA
Katika maandalizi ya Mashindano ya Nchi za KiAfrika hapa Bangalore yaendeleayo, Uongozi mzima wa TASABA ulisimama kidete kuhakikisha timu zote zapewa vifaa vyao muhimu kwa ajili ya mashindano hayo walau week moja kabla ya mashindano kuanza na hivyo ndivyo ilivyofanyika.
Wadhamini wakuu wa mashindano haya jana walihudhuria kikao kilichoitishwa na ungozi na macaptain na timu zote shiriki na kuweza someana sheria za mashindano, ratiba ya mashindano na pia kukabidhiana vifaa vyote muhimu, ambapo timu zoote zilipewa jezi ya kaptula, ya juu na soksi pamoja na kitambaa cha kapteni kwa kila timu, kitu kilichokua mojawapo ya makubaliano ya uongozi wa TASABA na Union of African Communities.
Tunaomba kusisitiza ieleweke kuwa TASABA ndio main Organizers wa Mashindano haya, na Union of African Communities in Bangalore ni wadhamini tu.
Tunapenda itakia timu yetu kila la kheri katika maandalizi ya mashindano hayo, wafike fainali na kuhakikisha kikombe kinabaki TASABA na wawafurahishe wa Tanzania nasi Uongozi tutajitahidi kuwa nao bega kwa bega.
Vifaa hivyo vya michezo viko chini ya Uongozi wa TASABA na uongozi wa timu chini ya Meneja Jerome na mkuu wa nidhamu Big Willy watakabidhiwa vifaa hivyo jhivi karibuni. Na mara baada ya mashindano hayo vifaa hivyo VITAPASWA KURUDISHWA NDANI YA HIMAYA YA UONGOZI WA TASABA, havitakua mali za watu binafsi kila mchezaji kuondoka nazo.
TUSHIRIKIANE PAMOJA KULETA KOMBE HILI NYUMBANI.
0 comments:
Post a Comment