Jiji la Dar es salaama siku ya ijumaa lilikumbwa na tetemeko dogo la richta 4.8 (magnitude 4.8) na kusababisha kizaa zaa kwa wakazi watumiao majengo marefu mara baada ya wao kuishia yakimbia makazi yao hayo..
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma alisema kuwa tetemeko hilo lilitokea saa 5:28 asubuhi katikati ya Bahari ya Hindia katika kina cha kilometa 10, umbali wa kilometa 52 kusini mashariki mwa Dar es salaam na kilometa 105 kusini mashariki mwa Zanzibar.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Faustine Shigole alisema, " Tumepata taarifa za tetemeko la ardhi, lakini hakuna taarifa yoyote ya uharibifu wa mali, wala vifo na hali imekuwa shwari"
Aidha watu wafanyao shughuli za baharini, wametahadharishwa kuwa makini mno kwani haijulikani kama tetemeko hilo ndilo la mwisho ama, kwani yameshapiga jiji letu kwa mara ya pili ndani ya miezi 6.

Kwa habari zaidi na picha tembelea blog ya Issa Michuzi ya http://www.issamichuzi.blogspot.com/
1 comments:
http://earthquake.usgs.gov/earthquakes/eqarchives/last_event/world/world_tanzania.php
Post a Comment