Ads 468x60px

Pages

Sunday, February 7, 2010

FEDHA ZA EPA.


Mpaka sasa hivi serikali imefanikiwa kuokoa kiasi cha fedha kipatacho bilioni 72 za kitanzania kutoka kwenye matumizi mabaya ya Benki kuu ya Tanzania kutoka kwenye kitengo cha Tanzania's External Payments Arrears(EPA)AMBAPO bilioni 19 kati ya hizo zilipatikana baadae.
Waziri wa wizara ya fedha na uchumi Mh.Mustafa Mkulo alisema kwamba bilioni 72 hizo ni kati ya zile bilioni 133 ambazo zilitumika kwa matumizi mabaya.
Wadau mabalimbali wameomba fedha hizi zitumike kwa ajili ya mipango endelevu ya nchi yetu na pia kuomba serikali kuwa makini ili zisije zikatumika vibaya tena na kusababisha turudi tilipokuwa mwanzo.
Matumizi mabaya ya fedha ambayo yanaambatana na uzembe na ubinafsi wa watu wachache umekua ukiweka nchi yetu kwenye hali ngumu kiuchumi ukilinganisha na nchi nyingine za dunia ya tatu zinazojaribu kujikomboa kiuchumi.
Wadau wameomba serikali kuwa waangarifu na mikataba wanayofanya isije ikaiweka nchi katika matatizo na kusisitiza kwamba waliohusika na matumizi hayo mabaya ya fedha wachukuliwe hatua za kisheria.

0 comments:

Post a Comment