Ads 468x60px

Pages

Saturday, February 6, 2010

WATANZANIA WA BANGALORE

HABARI KAMILI KUTOKA KWA RAIS WA TASABA KUHUSU HALI ILIVYO KWA SASA
BANGALORE – INDIA

Ndugu wanajumuiya wa TASABA, waTanzania wote kwa ujumla muishio India na mahali kwingine kote. Kutokana na kifo cha mwenzetu marehemu Imran Mtui kumekuwa na habari nyingi za kizushi. Taarifa kamili kuhusu chanzo cha kifo cha marehemu Imran Mtui kama tulivyoipata kutoka kwa vyombo vya dola hapo awali haina mabadiliko yoyote yale mapaka sasa. Kumekuwa na habari za kizushi zinazosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia simu za mkoni kuwa kuna raia wengine wawili kutoka Ivory cost wamekutwa wamekufa na habari hii ni ya uongo. Mimi binafsi nimeongea na Rais wa jumuiya ya waIVORY COST amekanusha juu ya habari hiyo ambayo imezagaa sana katika mji huu wa Bangalore-India. Naomba tuache habari hizi za kizushi kwani watu wanazipokea tofauti na wengine wanazitumia kama njia ya kujipatia fedha. Naomba tukumbuke kuwa kusambaza habari kama hizi za kizushi hapo baadae zitatupa shida sana kwani tunajijengea mazingira magumu sisi wenyewe. Habari za kizushi kama hizi zinachafua usalama wa nchi husika na kuiletea sifa mbaya kote duniani. Habari kama hizi zitazidisha chuki miongoni kwetu na wenyeji.Mambo mengi ambayo si taarifa rasmi yameandikwa na magazeti ya Tanzania na India kuhusiana na marehemu,tafadhali muacheni ndugu yetu apumzike kwa amani.Wakati huohuo nilikua ninawaomba tuwe watulivu tusubiri tamko rasmi toka ubalozi kuhusu chanzo kamili cha kifo cha marehemu Imran Mtui.
Fidelis Msomekela
Rais - TASABA

1 comments:

Anonymous said...

MR PRESIDENT tumekuelewa ila jamaa wanazingua hao huyu mshikaji kauliwa na ukweli ndo huo wakubali wasikubali ukweli utabaki kuwa huo!

Post a Comment