Ads 468x60px

Pages

Sunday, March 14, 2010

KUCHOMEWA NYUMBA MOTO KWA WANAFUNZI.

Tarehe 11/03/2010 majira ya saa 10:45 usiku walifika vijana 4 wakidai kuwa wamefanyiwa fujo na Wahindi kwa kurushiwa mawe na kupigiwa kelele za wizi. Vijana hawa walikuwa wanatoka nyumbani kwa wenzao ambako walikuwa wamekutana kupanga jinsi gani watakavyo wakilisha nchi yetu Tanzania katika sherehe ya ‘International Students Day’ itakayofanyika chuoni kwao Indian Academy degree college tarehe 19/03/2010, ndipo walipokuwa wakirudi wakakutana na Wahindi wawili waliokuwa kwenye gari wakiwa wamelewa ambao hupaki gari sehemu karibu na nyumbani kwa wenzao ambao ni; Hamis Mbelwa Fintan mwenye passport No. AB329730 na Olais Alexendra Siarra mwenye passportNo. AB329755waliokuwa wanakaa No.1093/1.11th Cross,Swarnanagar,Robertsonpet,KGF-563 122. Wahindi hao waliwasimamisha vijana hao wakitaka kujua walikuwa wanatoka wapi muda huo wa saa 10:30pm na kama wana vibali vya kuishi nchini, walipogundua kama walikuwa wamelewa waliwapuuza na kuendelea na safari yao, bila kujua kilichokuwa kinawatokea wale wahindi wawili walianza kupiga kelele na baadhi ya majirani kutoka na silaha kama, marungu, nondo na kuanza kuwakimbiza huku wakiwarushia mawe, kwa bahati nzuri hakuna majeruhi. Walipofika kwangu walinielezea kilichotokea nikawasihi wakae kwangu wasitoke mpaka pale hali itakapokuwa shwari. Tukiwa ndani mnamo majira ya saa 11:30pm Olais Alexendra Siarra alinipigia simu kunitaarifu kuwa wale wahindi bado wamekusanyana katika nyumba wanayoishi na wanataka wavunje mlango niliwasihi wasifungue huku nikiwa natafuta jitihada ya kuwasiliana na police, muda si mrefu Hamis Mbelwa Fintan alinipigia simu akinieleza kuwa wale wahindi wamemwaga mafuta ya petrol mlangano kwao na dirishani kisha wakawasha moto, moto ulifanikiwa kuwaka malangoni na kupenya ndani ambako walifanikiwa kuuzima ule wa ndani ukiwa wa nje unaendelea kuwaka. Majirani wanaokaa nyumba moja walitoka na kusaidia kuzima ule wa nje. Bahati nzuri petrol haikua nyingi na hakuna aliyejeruhiwa.

Nilitoka nikatafuta njia ya kufika kituo cha Police cha Hennur Cross, nilitoa taarifa hiyo wakatoka maafisa wa police na kufika sehemu ya tukio wakati huo mimi nikiwa nimebaki kituoni. Baada ya dakika 30 police walirudi bila watuhumiwa, nilpouliza walinijibu nirudi nyumbani wameshawatuliza na hawatarudia tena nilibishana sana na police juu ya hilo maana walipofika waliwakuta watuhumiwa na kuwaachia waende huru. Nilizidi kupigania haki lakini walinijibu “This is India not Tanzania and we have to coup with them like or not” niliwauliza kama huo ndio utamaduni wao wa kumwagia watu petrol na kuchoma moto kutaka kuwaua? Wakasema kama naona hawajanisaidia niende kutafuta msaada mahali pengine. Nilisikitika sana kwa kauli za police hasa ukizingatia kuwa toka Imran Mtui afariki ni mwezi tu na siku 6 mpaka sasa na hatujapata taarifa ya kuridhisha kutoka kwa police halafu linatokea jaribio linguine la kuua kwa kutumia petrol. Mh. Balozi hali hii inanitisha hasa nikiwa kama mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi kuona raia wenzangu wanatishiwa kutolewa maisha yao kwa moto na bila hatia huku police wakiona jambo hilo ni la kawaida kwao na kuwaachia watuhumiwa waende huru. Watu hawa wanaishi nchini kwetu kwa amani na kufaidi matunda ya uhuru na uchumi wa nchi yetu bila bugudha. Naomba ofisi yako teule iingilie kati suala hili leo hii walikuwa na petrol kidogo siku nyingine itakuaje?

Baada ya kuona hakuna masaada niliwashauri Hamis Mbelwa Fintan na Olais Alexendra Siarra wahame mahali pale kwani hapana usalama tena. Tulimtafuta landlord na kuongea nae akakubali kurudisha Deposit yao na kwa sasa wamehama wanaishi na rafiki zao huku wakitafuta nyumba nyingine. Hii ndo hali halisi inayotukuta raia wa Tanzania tusomao huku Bangalore. Ni matumaini yangu kuwa tutapata msaada wa kutosha kutoka ofisi za Ubalozi.

Natangukiza shukrani zangu za dhati,

Fidelis Msomekela

Mwenyekiti - TASABA

2 comments:

Anonymous said...

Tunashukuru mheshimiwa Rais wetu kwa kazi kubwa unayofanya ukishirikiana na jamii nzima ya watanzania wanaoishi Bangalore - India. Hili swala ni kubwa na ni la kutisha sana hasa ukizingatia kwambwa jamii ya Watanzania na waafrika kwa ujumla ni kubwa hapa japo kuwa si kama walivyo wenye nchi yao. Ombi langu ni kwamba hivi vitu vinavyotokea huku vinashtua nyumbani hasa wazazi wetu waloiko mbali, cha msingi ni kwamba tungependa kama vyombo vya habari vya huko vingekuwa vinapata habari kamili kuhusu tukio lolote linalotokea hapa kabla ya kutoa ktk habari zao kwa sababu saa zingine wanatoa habari za uongo tofauti na sie ambaao ndio wahusika tuliopo huku tunavyojua. na kitendo hicho kinawafanya wazazi na walezi huko kuwa na pressure kuhusu usalama wa watoto wao.

Tapeli said...

Sisi wazazi tunatoa shukrani zetu za dhati kabisa kwa msaada mnaoutoa kwa watoto wetu waliopo hapo Bangalore. Pia nawapa poleni sana kwa kazi ngumu kama hii. USHAURI wangu ni kuwa yanapotokea mambo kama haya ya kuchomewa nyumba na kutaka kuwaua watoto wetu hakikisheni habari hizi ninafika hapa nyumbani na kuandikwa katika magazeti ili tupate habari haraka. Vitendo vya kishenzi kama hivi vinaweza kusababisha na sisi kulipiza kisasi kwa wadosi walioko huku, maana wako wengi sana hatushindwi kuwafanyia unyama. Kwa mara nyingine tena poleni sana na MUNGU awape roho ya kusaidiana. Ila kama mambo yanawashinda semeni tu na sisi tufanye kazi huku. TAPELI

Post a Comment