Ads 468x60px

Pages

Monday, March 22, 2010

UFUMBUZI WA TUKIO LA KUCHOMEWA NYUMBA MOTO KWA WANAFUNZI.

Wanafunzi wawili ambao ni Ndugu. Hamis Mbelwa Fintan na Ndugu.Olais Alexendra Siarra, waliokuwa wanakaa Hennur Cross ambao walikutwa na mkasa wa kuchomewa moto nyumba yao wakiwa ndani umepatikna ufumbuzi baada ya Ubalozi wa Tanzania nchini India kuingilia kati sula hilo. tarehe 18/03/2010 Mh. A.M.R Mwamanenge kutoka ofisi za ubalozi wa Tanzania New delhi- India aliwasili jijini Bangalore. Majira ya 1:00pm siku hiyo hiyo tulifika katika kituo cha polisi cha Hennur Cross tukiongozana na Mh. A.M.R Mwamanenge na kuonana na Inspekta wa kituo hicho ambaye alitupa maafisa wawili wa polisi ambao tulifika nao sehemu ya tukio ili kujionea wenyewe kilichokuwa kimetokea na hatimaye kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha kituo cha polisi cha Hennur Cross. Watuhumiwa walipohojiwa hawakuwa na sababu ya msingi ya kueleza kisa kilicho wapelekea kufanya kitendo walichokifanya zaidi ya kuomba msamaha na kudai kuwa walikuwa wamelewa siku hiyo. Walikili kosa mbele ya Inspekta wa kituo hicho kimaandishi kuwa hawatarudia tena kosa hilo na pia kama itatokea tukio lingine kwa kipindi hiki basi wao ndio watakuwa watuhumiwa wa kwanza.
Ili kuweka hali ya amani na utulivu nikiwa kama mwenyeketi wa jumuiya ya waTanzania waishio Bangalore pamoja na wahanga wa tukio hilo tulimwomba Mh. A.M.R Mwamanenge tulimalize tatizo lile kwa njia ya diplomasia kwa kuwa kuwafungulia kesi na kuwapandisha mahakamani ingeweza kuleta mgogoro zaidi na wenyeji wa nchi hii pia ingechukua muda mwingi kushughulika na masuala ya mahakama wakati kesi ikiendelea hasa ukizingatia sisi ni wanafunzi . Tulimwomba Mh. A.M.R Mwamanenge atusaidie kutafuta njia ya msingi amabayo itatufanya tuishi kwa amani na kupata msaada wa polisi kwa haraka mara tutoapo taarifa ambazo zinaitaji msaada wao.Watuhumiwa walikukubali kulipa fidia ya kiasi cha 18,000Rupees ambazo vijana hao walitozwa na mwenye nyumba kufidia uharibifu wa mlango.
Tarehe 19/03/2010 nikiwa kama Mwenyekiti wa jumuiya ya waTanzania waishio Bangalore (TASABA) niliongozana na Mh. A.M.R Mwamanenge mpaka ofisi za High Commissioner wa polisi Bangalore na kuonana na Msaidizi wa Commissioner wa polisi Bangalore na kumweleza juu ya suala hilo na hatua zilichokuliwa kwa malengo ya kuzidisha usalama wa waTanzania waishio Bangalore- India, alitupa mikakati ya jinsi watakavyotusaidia kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India. Tulifika pia kwa Inspector General of Police wa Bangalore na kumjulisha pia juu ya suala hili. Hivyo kwa sasa ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na jeshi la polisi watapanga mikakati ya kuhakikisha kuwa amani na haki inatendeka kwa wananchi wa kiTanzania waishio Bagalore- India.

Ushauri wangu kwa waTanzania wale wanaotaka kuja kusoma Bangalore-India katika fani mbalimbali, wakati wanapotuma maombi ya shule au wanapotafuta shule/ vyuo wawasiliane na Mwenyekiti wa jumuiya ya waTanznia waishio Bangalore- India (TASABA) ili wapate msaada wa kimaelezo juu ya vyuo wanavyotafuta. Hii itasaidia kuwaweka waTanzania wasomao huku kwa pamoja na pia kuwatafutia makazi sehemu ambazo hazina fujo na za usalama zaidi kwao ili pale wapatapo matatizo wakiwa wanaishi sehemu moja kwa ukaribu zaidi wapate kusaidiana kwa njia moja au nyingine.Nawasihi pia wale wote waishio Bangalore na kwingine kote nchini India kuzingatia sheria na kanuni za nchi husika na kujiepusha na vyanzo vyote vinavyopelekea fujo kutokea.

kwa niaba ya waTanzania waishio Bangalore na uongozi wa TASABA, tunakushukuru sana Mh. Balozi kwa msaada tulioupata wa kuleta amani baina yetu na wenyeji wa eneo la Hennur Cross, na mikakati iliyowekwa kuhakikisha kuwa tunaishi kwa amani na kupata haki pale tutakapo pata matatizo. Pia namshukuru Mh. A.M.R Mwamanenge kwa kushirikiana nasi bega kwa bega kuhakikisha haki inapatika na kuleta amani na ulewano baina yetu na wenyeji hao na kutujengea nafasi nzuri ya kusikilizwa matatizo yetu mara tufikapo katika kituo cha polisi, ni dhahiri kuwa kwa sasa waTanzania waishio Hennur Cross/ Bangalore wataishi kwa amani. Naomba tuzidi kupata msaada kama huu au zaidi mara kwa mara pale tupatapo matatizo ambayo yatakuwa nje ya uwezo wetu kuyatatua.


Fidelis Msomekela
Mwenyekiti – TASABA
+919742176980

0 comments:

Post a Comment