Ads 468x60px

Pages

Wednesday, November 4, 2009

MTAZAMO WA WANAJUMUIYA JUU YA UONGOZI MPYA WA TASABA






MAONI YA MUHESHIMIWA RAIS MSTAAFU BARAKA ABDALLAH KANGE JUU YA UONGOZI MPYA.

"Ahsanteni.
Nimatumaini yangu kuwa baraza hili lililotangazwa na uongozi huu wa 2009/2010 chini ya Ndugu rais Fedelis Msomekela litaendeleza yale mazuri yaliyoachwa na uongozi uliopita,akinipigia simu kunijulisha hilo ndugu rais nilimwambia tunahitaji mudumishe umoja uliopo kati yetu sisi waTanzania wa Bangalore,
nawapongeza kwa baraza lenu zuri, mimi limenipa imani kwamba waliochaguliwa watawajibika vizuri sana katika kazi zao,niwapongeze kwa hilo kwanza.
Baraza limezingatia kanuni za jumuiya yetu ya Tasaba tokea ilipoanzishwa 2002 chini ya uongozi wa Ndugu rais Onesmo,napia naamini litaendeleza yale mazuri yaliyofanywa na awamu zote tatu,ya kwanza ya rais mstaafu ndugu Onesmo,ya pili ya rais mstaafu Ndugu Policarp Ndekana,ya tatu ya rais mstaafu Baraka Abdallah Kange na hii ya nne ya ndugu rais Fedelis Msomekela.
mimi nimekalia kiti hicho kwa muda mrefu,nafahamu ugumu wa kuongoza jumuiya kubwa kama hii yetu hapa Bangalore,ndugu yangu Aldo kamugisha unawajibu mkubwa sana kuhakikisha viongozi wa chini yako hawakuangushi katika utekelezaji wa kazi zenu,wakikusumbua.... wewe huna ubia nao,wawajibishe tu.
nitatoa ushirikano wangu wote kwenu,nikiamini katika misigi ya wakombozi wetu kama Marehemu Mwlm Julius Nyerere,marehemu Sheikh Abeid karume, marehemu mzee Shaaban Robert na wengine wengi.
niwatakie kila la kheri katika safari yenu ndefu mlioianza hivi kariburi,ninasema safari njema.....huwa inanipa shida sana kusema abiria mmoja akioza wote wameoza..ah ah huwa siamini katika hilo pia huwa mimi sisemi msafiri kafiri bali huwa nasema msafiri kakiri.
nikiwa namalizia kutoa maoni yangu nimepokea simu kutoka Mysore rais mstaafu Ritha Chokala akiniambia habari za wenzetu huko,nimemwambia tuko pamoja katika hilo...sisi kama waTanzania,amenihakikishia ushikrikiano wa kutosha katika uongozi mpya wa Bangalore 2009/2010.

aluta contineour....
"

MTAZAMO WA WANAJUMUIYA MBALIMBALI JUU YA UONGOZI MPYA.

Sancho Samuel,Dayandasagar College "kwa hali ninavyoiona naamini tutafika na serikali yetu mpya nachoomba iwe ya uwazi na ukweli"

Reward Elias,Dayanandasagar College "kazi inafanyika tujitahidi tuwasaidie viongozi wetu"
kama una maoni au maswali juu ya uongozi mpya tuma mtambalike@yahoo.co.uk

0 comments:

Post a Comment