Ads 468x60px

Pages

Friday, January 1, 2010

TAARIFA YA MSIBA


TANZANIA STUDENTS ASSOCIATION IN BANGALORE

(TASABA)
HABARI ZA MSIBA.

Naungana na waTanzania wenzangu katika kuomboleza kifo cha mzee wetu mpendwa Rashid Mfaume Kawawa
Mzee wetu “SIMBA WA VITA” amefariki leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. Mzee Rashid Mfaume Kawawa alizaliwa mwaka 1926 huko Liwale. Amekuwa mpiganaji hodari wa maendeleo ya Taifa letu katika kutetea haki na maslai ya waTanzania kuanzia Januari 22, 1962 alipokuwa waziri mkuu. Daima tutakumbuka mchango wake katika Taifa letu na daima atabaki kuwa mfano wa kugia katika vizazi vijavyo. Kwa niaba ya waTanzania wote waishio Bangalore- India natoa salamu zangu za rambirambi kwa familia ya hayati mzee wetu Rashid Mfaume Kawawa, kwa serikali yetu ya Tanzania na kwa waTanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mzee wetu mahali pema peponi Amin.
Fidelis Martine Msomekela
President of Tanzania Students Association Bangalore (TASABA)

1 comments:

Anonymous said...

inna lilahi waina ilaihi raajiuun,ni mzee wetu tutaendelea kumkumbuka kwa michango mizuri aliyoiachia taifa letu la Tanzania.

Post a Comment