Ads 468x60px

Pages

Monday, February 21, 2011

FISA-B’s FOOTBALL TOURNAMENT YAMALIZIKA VYEMA

Mashindano ya mpira wa miguu ya The Federation of International Students Association in Bangalore yaliyokuwa yameandaliwa ki vyuo yalifikia kilele chake jana kwa mechi ya kuvutia ya fainali iliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Christ, Koramangala baina ya timu za Christ University na Garden City College.

Mechi hiyo ilikua ya vuta ni kuvute ambapo hadi kipindi cha kwanza kinaisha, GCC walikua wanaongoza kwa goli moja lakinii Mpaka Refarii anapuliza Kipenga cha mwisho GCC walikua wana magoli manne huku Christ University wakiwa hawajajibu hata moja.

Tanzania ilipata bahati ya kuwakilishwa na WaTanzania watatu wasomao chuo cha GCC katika mechi hiyo ya fainali ndugu Kainkwa, Abuu na Uthman na pia Uongozi mzima TASABA uliwakilishwa vyema na wawakilishi wake wa TASABA ( Ndugu Hartman, bi Mariam, bi Mwamini, bi Magdalena na bi Eunice J) pamoja na Makamu wa Rais (Anase) na Mweka Hadhina (Vince) mara baada ya kupata mwaliko toka FISA-B, huku Rais na Katibu wa TASABA wakihudhuria vikao vingine.

Uongozi unapenda wapongeza GCC kwa ushindi wao hasa WATANZANIA wale watatu kwa kuipeperusha vyema bendera yetu, na sasa tuelekeze nguvu zetu zoote kuipa moyo timu yetu ya Tanzania kwenye tournament yetu itarajiwayo kuanza jumamosi.

Mungu Ibariki TASABA,
Mungu ibariki TANZANIA..

0 comments:

Post a Comment