Ads 468x60px

Pages

Monday, February 21, 2011

TUIPE SUPPORT TIMU YETU YA TANZANIA

Uongozi wa TASABA unawaomba wa Tanzania woote wasomao na kuishi Bangalore kujitokeza kwa idadi kubwa kuja ipa support, kuitia moyo na kuishangilia timu yetu pindi itakapokua inacheza mechi zake mbali mbali ili kusaidia nchi yetu kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Tunaombwa kujitokeza kwa wingi kwani kutakua na usafiri wa kwenda viwanjani Christ University, Koramangala na wa kurudi katika pick up point mtakazo kuwa mnachukuliwa mara baada ya nyie kutuhakikishia uwepo wenu.

Pia tunawaomba wale waishio karibu na maeneo ya viwanja hivyo kujitokeza kwa wingi uwanjani pasipo kusubiria usafiri au kusukumwa na UONGOZI, na kwa wale wenye kujisikia kuisaidia timu yetu kwa namna moja au nyingine ikiwemo ya michango mbalimbali ya vifaa,dawa,fedha au hata ya kimawazo tunawakaribisha sana, milango I wazi kuwasikilizeni na kushirikiana nanyi.

Tunawaomba wachezaji wetu nao wafanye mazoezi kwa bidii ili waipeperushe vyema bendera yetu ya Tanzania.
Hizi ni mechi za Tanzania kwa siku ya jumamosi na jumapili Christ university.

Jumamosi tarehe 26, saa tano unusu asubuhi, Tanzania itakipiga na Ivory Coast

Jumapili tarehe 27, saa nne asubuhi, Tanzania itapambana vilivyo na Congo

Jumapili tarehe 27, (siku hiyo hiyo) ila saa nane mchana, Tanzania itamaliza dimba na Nigeria.

Ndugu wa TANZANIA, tusikose mechi hizi nzuri na za kuvutia kwani ndio wasaa wetu kujumuika pamoja na kujivunia UTanzania wetu, tusiwe tu twakutana sehemu za starehe na misibani.

Mungu ibariki TASABA,
Mungu ibariki TANZANIA…

0 comments:

Post a Comment