Ads 468x60px

Pages

Tuesday, March 8, 2011

HAYAWI HAYAWI, YAMEKUA...TANZANIA MABINGWA WA TASABA CUP OF AFRICAN NATIONS.

Hatimaye timu kabambe ya wanafunzi wa Tanzania wasomao Bangalore, ilifanikiwa kutwaa kikombe cha mashindano "TASABA CUP OF AFRICAN NATIONS " (T-CAN) baada ya kuwatungua wa Cameroon kwa mikwaju ya penalti 5 kwa 4, baada ya mechi kuisha kwa sare ya mabao 2 - 2..

Mpambano huo ulikuwa wa kukata na shoka, ambapo timu zote zilikuja na mashabiki wake wa kutosha kuzipa nguvu timu zao ili ziweze kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Ilikua ni Cameroon iliyojipatia bao la kuongoza katika dakika ya 29 ya mchezo kwa njia ya shuti kali lakini katika dakika ya 34 ya mchezo, Tanzania ilisawazisha mara baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Cameroon kutokana na kona iliyochongwa kiumaridadi na winger Muddy, ambapo Kiungo Jaffar alipiga kichwa kilichogonga mwamba na mshambuliaji hatari Freddy akaja umalizia kwa kichwa.

Hadi mapumziko, mpira ulikua 1 - 1..

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya ajabu na dakika ya 60 ya mchezo, Tanzania ikajipatia bao lake la pili kupitia kwa kiungo wake Jaffar kwa shuti kali na la mbali lililomshinda golikipa wa Cameroon.Mara baada ya hapo Cameroon wakaanza mchezo wa rafu na wakabahatika kujipatia bao la kusawazisha katika dakika ya 83 ya mchezo huku Watanzania wengi wakiamini walishashinda kiurahisiii mechi ile ngumu.

Sare hiyo ilidumu hadi penalti ambapo Tanzania ikaanza vibaya penalti hizo kwa kiungo wetu Jaffar kuipaisha penalti yake. Huku Cameroon wakikosa penalti yao ya tatu, baada ya Golikipa wetu wa akiba na mahiri "Mpemba" kudaka. Penalti zingine za Tanzania zilipigwa Captain Freddy, captain msaidizi Khalidi Litoto, Rapha, Kevoo, Beki wa kati wa kutumainiwa Ramson ambopo wote walifanikiwa kufunga penalti hizo.Cameroon walikosa tena penalti yao ya mwisho na hivyo kuwafanya Tanzania kutawazwa kuwa mabingwa wapywa kwa mwaka 2011 - 2012...

Mara baada ya mchezo huo, Kocha wa timu bwana J.J Mapesa alipenda ushukuru Uongozi wa TASABA kwa kuwaamini sana yeye na Mwalimu wa nidhamu na kuwakabidhi timu, na alipenda washukuru watu wote walioshiriki kutafuta ushindi huu kwa njia moja au nyingine mpaka tukafanikiwa kuupata.

Pia mwalimu wa Nidhamu Bwana William ( Big Willy) alifurahishwa sana na juhudi za wachezaji na kuwapongeza na aliwashukuru Viongozi wa TASABA na Watanzania wote kwa ujumla kwa ushirikiano waliouonesha.

Blog yetu ilifanikiwa kuongea na rais wa TASABA, bwana Jumanne ambaye yeye aliweza kuweka majigambo kidogo tu juu ya juhudi za uongozi wake kwa mwaka huu na kuelezea kuwa ma Rais wote waliopita walijitahidi kutafuta kombe hili wakashindwa , lakini uongozi huu ulikuja na mbinu tofauti mbadala ikiwemo za kukabidhi timu kwa makocha na watu wa nidhamu na kujitahidi kufuatilia mazoezi ya timu kwa ukaribu sana, na matokeo yake nadhani kila Mtanzania ameyaona.
Pia alipenda washukuru Watanzania wote wa Bangalore kwa umoja walionyesha wakati wa mechi hizi na moyo wao wa kujitolea hasa wachezaji, na pia Viongozi wenzake wote waliojitolea wakati wote wa maandalizi ya mashindano haya mpaka yalipofikia kilele chake juzi.
Kapteni wa timu Freddy, akinyanyua kombe la ushindi juu mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.



Huu ni mwanzo tu, timu za mpira za Mysore, Hyderabad na kwingineko zikae mkao wa kuja nyolewa, kwani ukiona mwenzio ananyolewa...nawe tia kichwa maji!!!!!

MUNGU IBARIKI TASABA,
MUNGU IBARIKI TANZANIA,
MUNGU IBARIKI AFRICA.......

0 comments:

Post a Comment