Ads 468x60px

Pages

Friday, March 4, 2011

MAZOEZI YA TIMU YA TANZANIA YAPAMBA MOTO




Kuanzia jana, timu yetu ya Tanzania ilianza mazoezi yake tiyari kabsaa kupambana na Sudan katika mechi ya nusu fainali hapo kesho mara baada ya mapumziko mafupi ya siku tatu waliyopewa baada ya kufululiza mazoezi kwa muda na mechi kuwa nyingi kwa wakati mfupi ili kuponya majeraha, japo wakaangukiwa na bahati ya show ya Ay kufanyika katika kipindi hicho cha mapumziko.


Baadhi ya Wa Tanzania waliojitokeza kuja ipa support timu yao mwanzo mwisho,sio tu kwenye mechi bali hata mazoezini kama waonekanavyo bwana Msei, Arnold na Geroge hapa..

Uongozi mzima wa TASABA ulikua bega kwa bega na timu hata katika mazoezi, baadhi ya siku uongozi mzima ulihudhuria mazoezi hayo bila kujali umbali, kama waonekanavyo hapa rais,mweka hadhina na viongozi wengine.

Mvua ilikuja,lakini haikukatisha tamaa wachezaji wetu kujifua, lazma wa Sudan watukome.

Sio mieleka hii, bali ni mojawapo ya tizi zito sana walilokua wakilipiga vijana wetu

Tizi hilo la kubebana likiendelea

Hapa sasa.......

Mweee..... yaelekea hili zoezi lapendwa zaidi na vijana wetu kuliko mazoezi mengineyo yoote

Mipira vichwa yoote itakua yachukuliwa na Tanzania kama kiwango cha urukaji kitakua kama cha Abbas, Litoto,Freddy na Mazin kama waonekanavyo kwenye picha hii

Wakinyoosha misuli..

Wakifanya zoezi la kupiga deki kidogo, yaani vijana wetu wako fiti

Muondoko wa umiss ukikolezwa

Hili tuliambiwa laitwa zoezi la kutembea kimiss..

Muongoza mazoezi wa captain msaidizi khalidi Litoto akionyesha kwa ufasaha zoezi zima la muondoko wa kimiss litakiwavyo kufanywa..sina uhakika na juu ya suala zima la uvaaji allstar na njumu nao ulitakiwa ufuatwe na wote au

Mashujaa wetu wa Tanzania wakijifua vilivyo

hapa wakila round yao ya 8 kama sio ya kumi kuongeza pumzi.


0 comments:

Post a Comment