Ads 468x60px

Pages

Monday, March 7, 2011

LIVERPOOL WAIGARAGAZA MANCHESTER UNITED


Timu ya Liverpool jana ilifanikiwa kuigaragaza vibaya mno Manchester united kwa kuwafunga mabao matatu kwa moja na hivyo kukwea hadi nafasi ya sita katika msima wa ligi kuu ya Uingereza.

Mabao hayo yalifungwa yote na Mholanzi Dirk Kuyt katika dakika za 34, 39 na 65, huku la Manchester united la kufutia machozi lilifungwa na Chicharito..

Ama kweli mpira unadunda siku zote, liverpool iliyokua kwenye the bottom 3 leo angalia iliko.


Muuaji wa Manchester united mashetani wekundu Dirk Kuyt akishangilia moja ya magoli yake ya jana huku Meireles akimfuata..

Dirk Kuyt akitumbukiza nyavuni moja ya mabao yake huku Carrick akichunguliwa kwa nyuma na Wes Brown akisindikiza kwa macho pamoja na Steven Gerald.

Aidha matokeo mengine ya ligi ya Uingereza jana jumapili ni kama ifuatavyo :

Wolves 3.....vs.... Tottenham 3


Defoe akifunga moja ya mabao yake

Mabao ya Wolves yalifungwa na Doyle katika dakika ya 20 ,Doyle tena akafunga kwa njia ya penalti katika dakika ya 40na Fletcher akawafungia wolves bao lililowapa point 1, dakika ya 87.

Huku ya Tottenham yakifungwa na Defoe dakika za 30, 35 na Pavlyuchenko dakika ya 48

0 comments:

Post a Comment