Ads 468x60px

Pages

Tuesday, March 8, 2011

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Leo ni siku ya wanawake Duniani ambapo duniani ,huadhimishwa kwa wanawake kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo, na pia hukutana kuweza kujadiliana mambo mengi yenye kuweza kuwasaidia wanawake wenzao.

Mwaka huu, siku hii inaadhimishwa kwa wanawake kuzidi kutaka usawa katika mambo yote ya kijamii na kimaendeleo, na pia wanawake wanaombea dunia iwe yenye amani na upendo.


Nchini Mmetu, siku hii inasherehekewa kwa Wanawake kufanya maandamano ya amani mpaka katika viwanja vya mnazi mmoja ambako kutakua na mkutano wao wa hadhara.

Wanawake wa rika zote wakiwa na mabinti zao, wakijadiliana mambo mbali mbali ya kuleta maendeleo huko Delhi, India

Hata Ulaya hii ni siku nzuri sana kwa wanawake wote kuwa pamoja, kuongelea mambo yao.


Uongozi wa TASABA, unawatakia heri ya sikukuu hii ya Wanawake duniani.

MUNGU AWAZIDISHIENI ROHO YA UPENDO!!





0 comments:

Post a Comment