Ads 468x60px

Pages

Thursday, March 3, 2011

TASABA CUP OF AFRICAN NATIONS { TCAN } KATIKA PICHA


Wanaume wa kazi Tanzania wakila jalamba tayari kwa mechi yao moja chini ya uongozi wa captain Freddy na captain msaidizi Khalidi Litoto


Viongozi mbali mbali waandaji wa mashindano haya wakipiga picha ya pamoja na wachezaji wa timu za Sudan na Cameroon kabla ya mechi yao..ambapo Sudan walishinda kwa goli moja


Wa Ivory Coast wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kupambana na Tanzania,mechi iliyoisha kwa suluhu.


Timu ya Rwanda wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Uganda, ambapo waliwafunga kwa goli moja lilifungwa na Leandre


Timu ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakiwa katika majadiliano ya hapa na pale wakati wa mapumziko ya mechi yao dhidhi ya Nigeria ambapo walilala kwa mabao mawili kwa moja


Wa Nigeria wakiwa na furaha tele mara baada ya kuwabanjua Congo kwa mabao mawili kwa moja


Wa Cameroon wakiingia uwanjani kwa mkwara mzito mnooo


Sudan nao hawakuwa nyuma,walikwepo kuwakilisha nchi yao


Ma official wa mechi zetu wakiwa katika picha ya pamoja... huku mmojawao akijaribu wasiliana moja kwa moja na fifa kuji update na mabadiliko yoyote ya sheria za mpira.

0 comments:

Post a Comment