Ads 468x60px

Pages

Tuesday, March 8, 2011

WASHABIKI NAO HAWAKUWA NYUMA SIKU YA FAINALI

Kama kawaida na desturi ya Watanzania walioko Bangalore chini ya Uongozi wa TASABA, waliendeleza desturi ya kujitolea kwa wingi kuja kuishangilia timu ya na kuipa moyo wakati ikicheza fainali za mashindano ya T-CAN....


Mwalimu wa nidhamu wa timu bwana William ( Big Willy ) akiongoza timu yake kushangilia ushindi mara baada ya mikwaju ya penalti kumalizika, ama kweli ilikua ni furaha iliyoje.


Watanzania wakishangilia ushindi, mara baada ya mchezaji wa Cameroon kukosa penalti ya mwisho.

Wa dada kutoka Kamanahali nao hawakuwa nyuma.

Mweka Hazina wa TASABA bwana Vince, ( Mwenye t-shirt nyekundu aliyechuchumaa )akiwa bega kwa bega na timu kama ionekanavyo hapa akifanya kazi ya kugawa maji ya kunywa na dawa za kupunguza maumivu.

Katibu wa TASABA bi Edna akiwa na Dj kutoka Kenya Dj- Charlie pamoja na wadada toka Banaswadi.

Washabiki walikua kila kona ya uwanja

Kocha wetu wa makipa bwana amiri akitoa maelekezo kwa Ustadhi wetu Mpemba namna ya kucheza na penalti..

Watanzania wa Bangalore walikua bega kwa bega na timu yao kuipa moyo kama waonekanavyo hapa wakati wa mapumziko..huku naibu waziri wa burudani bibi Eunice Frankie ( dada mwenye miwani) akiwa makini na idara yake

Benchi la kidedea lilikua makini na kazi yake mwanzo mwisho

Wengine tulitoka kanisani, moja kwa moja kufika uwanjani kwa kutotaka kupitwa na tukio hili la kihistoria.

Mgeni rasmi raisi wa Umoja wa Waafrica Bangalore ( U.A.C.B ) bwana Jimmy akiwa pamoja na rais wa wa Nigeria Bangalore, na Rais wa wa Cameroon Bangalore.

Wa dada nao wakifurahia fainali kwa namna yao ya kipekee.

Kila mtanzania mzalendo siku hiyo ndani ya Bangalore aliacha shughuli zake zote na kuja kushuhudia mechi hii ya kihistoria

Rais mstaafu wa TASABA bwana Baraka Kange ( Mwenye shati la kijani ) akifuatilia kwa umakini pamoja na wa Tanzania wengine

Wa dada kutoka Indranagar nao hawakuwa nyuma kuipa moyo na kuishangilia timu yetu.

0 comments:

Post a Comment