Ads 468x60px

Pages

Saturday, March 5, 2011

WATANZANIA WA BANGALORE WAIBANJUA SUDAN 2 - 1 NA KUTINGA FAINALI KWA KISHINDO

Kikosi cha ushindi..

Timu ya Sudan

Timu ya Tanzania ikipiga dua, kabla ya mechi yao

Wachezaji wakipeana mawaidha ya hapa na pale..

Habari zilizoingia mitamboni muda si mrefu ni kuwa timu ya wanafunzi wa Tanzania wasomao Bangalore, wamefanikiwa kuingia kwa kishindo katika fainali za TASABA's Cup of African Nations baada ya kuitandika Timu ya sudan mabao mawili bila ya majibu.

Magoli hayo yalipatikana katika dakika ya 28 ya mchezo kwa njia ya penalti iliyopigwa kwa ufundi mkubwa na kiungo mahiri bwana Jaffar.
Sudan walizidi mchezo wa rafu na penalt ingine ikapatikana katika dakika ya 42 ya mchezo ila safari hii Golikipa wa Sudan aliweza otea penalti ya Jaffar na hivyo kufanya hadi mapumziko mchezo kuwa 1 - 0.

Kipindi cha pili Tanzania ilishambuliwa sana,ikafanya mabadiliko ya akili na Striker wake mahiri Fredy aliyeanzia benchi leo aliingia na kupachika bao la pili lililozima ndoto zooote za wa sudan kuingia fainali.

Hii ni mara ya pili katika historia ya Tanzania students Association ( TASABA) kwa timu yake ya mpira kuingia fainali za mashindano yoyote makubwa hapa bangalore ambapo mara ya kwanza ilikua mwaka 2008, ambapo tanzania ilifungwa na wa Ivory Coast.

Haya vijana wa 2011 tunaomba tuandike historia mpya ya kuwa wa kwanza kutinga fainali na kuchukua kikombe kikubwa hiki kwa mwaka huu.Hiyo ni changamote twawapeni.

2 comments:

Anonymous said...

ni mbili bila naomba ukosoe...

Anonymous said...

soma tena sentensi ni kuwa mpaka mapumziko ndio ilikua 1 - 0.
ila mpaka mpira umeisha ilikua 2 - 0 uko sahihi..

Post a Comment