Ads 468x60px

Pages

Tuesday, March 8, 2011

MECHI YA FAINALI ZA ( T-CAN ) KATIKA PICHA

Shughuli yetu ya Wa Tanzania - Bangalore kwenda mchukua mwali, ilianzia hapaaaa kwa washambuliaji wetu Freddy na Dullah kuanzisha mechi mnamo saa tisa alasiri

Hiki ndicho kikosi shupavu cha TASABA - Bangalore
( Waliosimama kutoka kushoto ) : Rais wa TASABA Jumanne, Ima, Rapha, Kevoo, Dullah, Mpemba, Mazin, kapteni Freddy, Kocha J.J. Mapesa, kapteni msaidizi Jaffar
( Waliochuchuma, kutoka kushoto ) : Tuma, Kapteni msaidizi # 2 Khalidi Litoto, Ramson, Muddy, Shaah, Junior na Harry..
Waliokosa picha hii : Hamisi, Yonna, Abbas, Uthman na Kainkwa wote kutokana na majeruhi

Washindi wa pili wa mashindano haya Cameroon wakisali dua kabla ya mechi ya fainali

Kikosi cha TASABA kikiimba wimbo wa Taifa lao la Tanzania kwa madaha makubwa

Wachezaji wakipewa huduma ya kwanza na muuguzi wetu wa timu, dada Edna ambaye pia ni katibu wa TASABA
Timu zote mbili zilizoingia fainali zilipiga picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa wa Africa walioko Bangalore ( U.A.C.B) na wasimamizi wa mechi hizo

Mgeni rasmi wa mechi ya fainali ambaye pia ni rais wa Umoja wa wa africa walioko Bangalore bwana Jimmy kutoka Congo akisalimiana na wachezaji wa Cameroon,akiongozwa na Kapteni wa Cameroon bwana Harrison

Mgeni rasmi wa mechi ya fainali ambaye pia ni rais wa Umoja wa wa africa walioko Bangalore bwana Jimmy kutoka Congo akisalimiana na mshambuliaji wetu Junior huku Kapteni Freddy akimtambulisha

Mgeni rasmi wa mechi ya fainali ambaye pia ni rais wa Umoja wa wa africa walioko Bangalore bwana Jimmy kutoka Congo akisalimiana na winga wetu maridadi Kevoo, huku Haryy na Muddy wakimsikilizia

Fair play ilitawala mechi nzima, kuanzia mwanzoni mwa mechi hadi mwisho kama ionekanavyo hapa

Wachezaji (Junior, Muddy, Ima, MAzin na Kevoo ) wakisikiliza maagizo ya mwisho mwisho toka kwa viongozi kabla ya mechi yao

Golikipa wetu mahiri wa akiba ambaye Ustadhi Mpemba akitafakari mambo huku wachezaji wengine wakita wakipasha kabla ya mechi

Wa cameroon wakipasha viungo vyao kwa ngoma zao maridadi kabla ya mechi

Ama kweli walikua ni watu waliojishibia na wenye miili yao, timu yetu kweli yastahili pongezi

Wa Cameroon wakivaa tayari kwa mechi yao mara baada ya kuwasili uwanjani

0 comments:

Post a Comment