Ads 468x60px

Pages

Monday, March 7, 2011

MAELFU WAFURIKA LOLIONDO KUTIBIWA MAGONJWA SUGU

Maelfu ya watu wamekua wakifurika Loliondo nyumbani kwake Mchungaji mzee Mwasapile kijiji cha Samunge tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro kupata dawa iitwayo " dawa ya maajabu ya Mungu" iaminikayo kutibu magonjwa mbali mbali sugu ikiwemo kisukari, pumu, saratani na hata Ukimwi



Mchungaji Mwasapile akihojiwa na waandishi wa habari, huku akiwa ameshikilia kikombe chake cha kipimo cha dawa.

Msururu wa magari kama uonekanavyo,watu wakipanga foleni ya matibabu

Mchungaji akiwapimia wagonjwa dawa,ambapo ni mwendo wa kikombe kimoja cha shillingi 500 tu,wapona magonjwa yako yoote

Watu wa kila kabila walikwepo kama hapa waonekanavyo wenye asili ya ki asia nao wamefunga safari kupata matibabu

Gari lenye namba za serikali SM 3178 nalo likiwa kwenye msafara wa kusubiria matibabu..



Helkopta za wafanyabiashara na magari zaidi ya 1000 yamekuwa yakimiminika kijijini humo, huku watu wa rika na race zote wamekua wakionekana kupanga foleni kupata tiba hiyo ambayo mchungaji huyo anasema alioteshwa na Mungu kuitumia tangia mwaka 1991.

Aidha anasema dawa hiyo inapatikana kutoka kwenye mti wa mugariga,ambapo ni yeye tu anaweza kukupatia na ukifuata masharti yake na kunywa kikombe kimoja tu, itaanza kutibu magonjwa hayo yoote sugu.
Dawa hiyo inatolewa kwa bei ya shillingi 500 tu..

Habari hii imeandikwa na Mussa Juma na Daniel Sabuni kutoka Loliondo..
Picha ni kwa hisani ya blog ya Amani Masue...

0 comments:

Post a Comment