Ads 468x60px

Pages

Monday, March 21, 2011

WANAFUNZI WA ST.GEORGE COLLEGE OF MANAGEMENT WAFANYA STUDY TOUR INDIA..

Wanafunzi wa kozi mbalimbali katika chuo cha St. George, Banaswadi, Bangalore wakiwemo wa Tanzania wanne ambao ni manaibu waziri wa TASABA wa Jamii na Burudani Bwana Jerome na bi Eunice Frankie, beki wetu wa kutumainiwa wa Tasaba Football team bwana Ima Paul na bibie Jescar..., walifanya safari ya kimasomo kutembelea miji mbali mbali India ambako waliweza kujionea vitu vingi, kutalii na kujifunza vitu vingi mno ambavyo wanaweza kwenda vitumia katika maeneo yao ya kazi pindi watakaporudi nyumbani mara baada ya masomo yao.

Walipata tembelea miji ya Pune, Mumbai na Goa wakiwa na walimu wao.
Walipata nafasi adimu za kuona sehemu za vivutioa kama The Mumbai gates, the Taj hotels, Viwanda vya Cocacola, Steel and metal industries na kiwanda cha Bia na maji cha Kingfisher.



Misosi wanasema ilikua ni ya uhakika, miili ama kweli haijengwi kwa mawe


Mara baada ya kutoka kiwanda cha Kingfisher Goa

Raha ya kuwa mwanafunzi sio tu kuhudhuria darasani, na unadhifu wa mwanafunzi nao unaongeza marks kama waonekanavyo mabwana hawa wawili..

Safari haikua ya masomo tu, bali na kuchangamsha akili na kupata uzoefu mpya kama waonekanavyo bwana Jerome na Ima,pia walitaka dhihirishia umma kuwa wao sio mpira wa miguu tu, hata uvuvi wanaujua..

Wakiwa nje ya the Mumbai gate pamoja na wanafunzi wenzao kutoka IvoryCoast na Ethiopia

Walipata bahati ya kutembelea hoteli za taj mahal ambazo ziliwahi shambuliwa na magaidi na sasa zimefanyiwa matengenezo kama ionekanavyo hapa..

Mapozi time, haya dole gumba juuuu....well done bwana mapesa

Wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kugusa ardhi ya Goa

Wakiwa kwenye ma pozi matata wakiwa mapumziko mara baada ya kutembelea mojawapo ya viwanda

Safari zoote zilianzia hapaa,wanafunzi wakiwa na nyuso za furaha wakiwa stendi mara baada ya kuanza safari..



0 comments:

Post a Comment