Ads 468x60px

Pages

Saturday, March 5, 2011

NUSU FAINALI ZA T-CAN KATIKA PICHA



Nusu fainali za kombe hili la waafrica wasomao Bangalore, zilichezwa leo katika viwanja vya Christ University, ambapo katika mechi ya kwanza timu ya Cameroon ilifanikiwa kutinga fainali kwa njia ya mikwaju ya penalti mara baada ya mechi yao kuisha kwa sare.

Cameroon walipata penalti 4 na wa Nigeria waliishia pata mbili, hivyo kuwa nchi ya kwanza kujikatia ticket yake kuingia fainali zitakazochezwa kesho.

Mara baada ya mechi yao, si wachezaji,si washabiki ilikua ni mwendo wa kucheza ngoma tu kama ionekanavyo hapa,kushangilia ushindi wao na kuingia fainali.

Wa Cameroon wakipiga dua kabla ya kuanza kwa penalti.

Hapa sasa ilibidi waachiwe kama nusu saa ya kuyarudi mangoma ya kwao,wakiwaacha wanigeria wakigombana kila kona na kila mtu kuondoka kivyake uwanjani wakati walikuja pamoja.

Hawa ndio wauaji wa Wa Nigeria ambapo, Ballack au Fanou Franklin ( Wa kwanza kushoto ) ndiye aliyekosa penalti, Zanga, Bah Terence, Hugues Nenengue, na Tataw George walizipata penalti zao zote, wakiwa katika picha ya pamoja na Captain wao bwana Harrison pamoja na Rais wa TASABA, bwana Jumanne ambao ndio main Organizer wa Mashindano haya.

Nigeria walikua hawaelewani kabisaa leo na walipata heka heka nyingi mno uwanjani.

Tunawapongeza sana wa Cameroon kwa kuweza ingia fainali ya Mashindano yetu haya, ila tu twapenda waonya kuwa cha moto watakiona siku ya fainali dhidi ya Tanzania.



0 comments:

Post a Comment