Ads 468x60px

Pages

Saturday, March 5, 2011

WASHABIKI WA KUMWAGA TU KWENYE MECHI YA TANZANIA

UONGOZI WA TANZANIA STUDENTS ASSOCIATION - BANGALORE unapenda washukuru Watanzania wote waliojitokeza kuanzia mwanzo wa mashindano haya mpaka sasa twafikia ukingoni,kuja ishangilia timu yetu na kuipa hamasa ari kubwa ya ushindi timu yetu pamoja na vipaji vya wachezaji hao.

Aidha Uongozi unapenda washukuru mno wachezaji wetu kwa kutufikisha fainali za mashindano haya, twawaomba tuzidishe juhudi na moyo wa kujitoa zaidi ili tuweze kubakisha kikombe hiki nyumbani.

Mwisho kabisa tunawaombeni wa Tanzania wote walioko Bangalore kesho tujitahidi kufika viwanja vya Christ University kushuhudia timu yetu ikitwaa kikombe hiki na kuishangilia kwa nguvu zote


Golikipa wetu wa siku ya leo Ustadh Mpemba akitafakari mawili matatu wakati wa mapumziko, kwa kweli leo ametuokoa sana na michomo mingi ya hatari ya wa sudan...big up kwako Mpemba

Naibu waziri wetu wa social na burudani bi Eunice F. akiwa na waziri wa Foreign affairs bi Alice K. na naibu waziri wa Elimu bwana Hartman wakiwa pamoja na Watanzania wengine kuipa support bab k.

Sio tu wa tanzania walikua wakiimba kama ionekanavyo hadi watu wa nchi nyingine nao walikuwa wana tuunga mkono kwa kandanda swafi lililokua latandazwa na timu yetu.
Viongozi wa ushangiliaji ambao waliweza watia hamasa kubwa na wengine kushangilia kwa nguvu zote wakati wote wa mechi, bwana Uthman Y. kiongozi wa TASABA kule Tc Pallya (mwenye miwani), pamoja na Ustadh Ali toka Hennur huku kwa mbaali Rais wa Tasaba mtoto kutoka Kariakoo akiendeleza kidedea uwanja mzima.

Washabiki wetu toka Acharya wakiwa pamoja na beki wetu shupavu Ramson mara baada ya mechi.


Makamu wa Rais mzee Professori nayeeeee..... akiwa na wadada toka kamanahali waliokuja ishangilia timu yao.

Salome, Rodgers toka banaswadi wakiwa pamoja na Chris mnigeria na George Mkenya ambao walikuja uwanjana maalumu kuishangilia timu ya Tanzania.

Wadada toka Banaswadi wakiwa tayari kwa mechi

Washangiliaji toka Tipsandra na Indranagar

Kulikua na washabiki hadi toka Mysore kama vile dada Glory aonekanavyo hapo,pamoja na dada Mwamini, wakiwa na Mheshimiwa Elinazi kiongozi wa tasaba, Tcpallya ambao walitokea kanisani moja kwa moja na kutia timu viwanjani.

Wadada toka Gubi nao walikwepo kuipa tough timu yetu.

Viongozi wa TASABA, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi pamoja na mwalimu wetu wa nidhamu.

TUNAWASHUKURUNI SAANA, NG'OMBE TUMEMLA MZIIIIMA KABAKI MKIA TU, HIVYOOOO TUUNGANE SOTE KWA PAMOJA KATIKA HIII SHUGHULI ILIYOKO MBELE YETU TUIMALIZE SWALAMA...

MUNGU IBARIKI TASABA..
MUNGU IBARIKI TANZANIA..


0 comments:

Post a Comment